kamati kuu ya CCM ilikaa jana siku ya jumatatu na kumchagua Dk Dalalay Peter Kafumu kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo wa Igunga,Tabora. Dk Kafumu ni kamishina wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini ambapo katika uchaguzi huo alipita kwa 68% kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye, uchaguzi huo unafuata baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kujiuzulu.
No comments:
Post a Comment