Tuesday, August 23, 2011

KATIBU MKUU KIONGOZI AMRUDISHA KAZINI KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI DAVID JAIRO


 
Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo akitoa taarifa kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Kitundu Jairo kufuatia tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wabunge tarehe 18 julai 2011 mjini Dodoma. kulia kwake ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Ludovick Utoh na aliyesiamama na wanahabari mwenye koti jeusi ni Mkurugenzi wa Habari Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu

Na Francis DandeKwa mujibu wa katika taarifa yake yenye kurasa nne Katibu Mkuu Kiongozi amesema kutokana na mamlaka aliyonayo kwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma, tarehe 21a bjulai, 2011, kwa kuzingatia uzito wa tuhuma alianzisha uchunguzi wa awali na kumpa likizo ya malipo Bwana Jairo ili kupisha uchunguzi.

Uchunguzi huo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Lodovick Utoah umeonyesha kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni julai 18 hazikuwa kuthibitishwa, kutokana na na matokeo hayo ya uchunguzi wa awali, “mimi kama mamlaka ya nidhamu ya katibu mkuu Nishati na Madini, Bw David Jairo, sitaweza kuendelea na hatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma (notice) na hati ya mashitaka kwa sababu bw. Jairo hajapatikana na kosa la kinidhamu (disciplinary offence) kwa mujibu wa taarifa maalum.

Amesema kufuatia matokeo hayo ya taarifa hii ya awali na kwa mamlaka niliyonayo kwa mujibu wa sheria namba 8 ya utumishi wa Umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003, NINAAMURU BWANA DAVID KITUNDU JAIRO AREJEE KAZINI KUANZIA SIKU YA JUMATANO TAREHE 24 AGOSTI 2011.Habari Kwa Hisani Ya Michuzi Blogu

No comments:

Post a Comment

hostgator coupon code