Friday, August 19, 2011
MAANDALIZI YA OLYMPIC 2012 NA SWALA LA USALAMA KATIKA JIJI LA LONDON
Ili kuakikisha swala la usalama linakuwa thabiti mashabiki watakao kwenda katika mashindano hayo itawalazimu kupanga foleni ya kufanyiwa ukaguzi utakao chukua takribani dakika 20, mkurugenzi wa maswala ya usalama katika michezo hiyo bwana Ian Jonston amesema wameweka X-ray za ulinzi takribani 300-400 katika kila geti la kuingilia katika airport za jiji hilo, naye mratibu wa mawala ya usalama katika michezo hiyo amesema kutakuwa na jumla ya maafisa polisi 10,000 na maofisa ulinzi 13000 wakiasaidiwa na maofisa usalama watakuwa wakizunguka katika eneo mbalimbali yatakayofanyika mashindano hayo. Hayo yote yanakuja ili kuakikisha wanawaondoa hofu mashabiki watakao hudhuria katika michuano hiyo kutokana na fujo zinazoendelea sasa katika jiji la London.
Hii ndo "Olimpic Park" katika mji wa Stratford, East Londan ambapo takribani watu 350,000 wanakidiriwa kuutembelea mji huo kwa siku wakati wa michuano ya Olimpic 2012,hapo ndipo ulipojengwa na uwanja wamichezo ya majini ambapo waingereza wanamtegemea kwa kiasi kikubwa mchezaji wao kijana mwenye umri wa miaka 17 Tom Daley kuwatoa kimasomaso.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment