Saturday, August 13, 2011

IDARA YA SANAA ZA MAONYESHO CHUO KIKUU CHA DODOMA

 

Mkuu wa idara ya sanaa chuo kikuu cha Dodoma DKk Nyoni akiongea na wanafunzi wa mwaka wa kwanza kabla hawajaanza kuigiza igizo la Nguzo mama toka katika kitabu kilicho andikwa na Penina Mhando, kama sehemu ya mitihani yao ya kumaliza mwaka wa kwanza wa masomo
Hapa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaochukua shahada ya kwanza ya sanaa za maonyesho katika chuo kikuu cha Dodoma wakiwa stejini katika mitihani yao ya kumaliza mwaka
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Dodoma akiigiza stejini
Walimu mbalimbali katika idara ya sanaa za maonyesho wakifuatilia vijana wao wakiwa stejini hatua kwa hatua na kutoa alama 'marks" kwa kila mwanafunzi.
Hiyo ndio hali halisi katika chuo kikuu cha Dodoma wanafunzi wakijituma kuongeza weledi katika vipaji vyao mungu alivyo wajalia

No comments:

Post a Comment

hostgator coupon code