Mwenyekiti wa Umoja wa Wake na Waume wa mabalozi wa nchi za Afrika waliopo nchini, Aletha Isaack (kushoto) akikabidhi funguo za gari la wagonjwa kwa Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya na
Serikali imesifu jitihada zinazochukuliwa na wake za mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini katika kuhakikisha vifo vya akinamama na watoto vinapungua.
Akizungumza wakati akipokea msaada wa gari la wagonjwa kutoka umoja wa wanawake hao jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Magreth Mbando, alisema nguvu zao zitaongeza kasi ya utoaji tiba huduma ya uzazi salama.
Gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 11 limetolewa kwa ajili ya kutoa huduma katika Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala.
Dk. Mbando alisema hospitali hiyo inawahudumia watu 29,000 katika huduma ya uzazi kwa mwaka ambayo ni wastani watu 60 hadi 100 kwa siku. Wagonjwa wanaopatiwa rufaa ya kwenda muhimbili ni kati ya watu watatu hadi sita kwa siku.
kwa hisani ya Nipashe
No comments:
Post a Comment