Watu zaidi ya 2,200 wameripotiwa kuuwawa katika fujo zinazoendelea nchini Syria zilizoibuka toka katikati ya mwezi March 2011,hayo ni kwa mujibu wa Kamishina wa maswala ya Haki za Binadamu wa U.N. Navi Pillay ambapo aliyazungumza hayo katika mkutano wa baraza la haki za binadamu iliyofanyika huko Geneva, Swatzerland ambalo lilikusudia kuzungumza swala la uvunjwaji wa haki za binadamu nchini Syria.Pillay alisema tayari watu zaidi ya 2,200 wameuwawa na zaidi ya watu 350 wameripotiwa kufa tangu kuanza kwa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment