Friday, August 26, 2011

BENKI YA NBC YACHANGIA KWA WANAMICHEZO WA TANZANIA WATAKAOSHIRIKI ALL AFRICA GAME


Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC Tanzania, Robi Matiki-Simba (kulia) akikabidhi tiketi saba za ndege za kwenda na kujrudi Msumbiji kwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Kanali Iddi Kipingu kwa ajili ya timu ya Tanzania ya wanamichezo wenye ulemavu inayotarajiwa kushiriki michuano ya Afrika ya All Africa Games nchini Msumbiji kuanzia Septemba 3 mwaka huu. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania, Iddi Kibwana.
Baadhi ya timu ya Tanzania ya Paralimpiki wakipozi kwa picha na Kanali Kipingu, Meneja Uhusiano wa NBC, Bi. Robi na Katibu Mkuu wa TPC, Iddi Kibwana katika hafla hiyo.
Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC Tanzania, Robi Matiki-Simba (kulia) akishikana mikono na mwanamichezo mwenye ulemavu, Bernadeta Kinyelo baada ya kukabidhi iketi saba za ndege za kwenda na kurudi Msumbiji kwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezom la Taifa (BMT) Kanali Iddi Kipingu (wane kulia waliosimama) kwa ajili ya timu ya Tanzania ya wanamichezo wenye ulemavu inayotarajiwa kushiriki michuano ya Afrika ya All Africa Games nchini Msumbiji kuanzia Septemba 3 mwaka huu. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment

hostgator coupon code