Sunday, August 21, 2011
ZIARA YA RAISI JAKAYA KIKWETE MKOANI LINDI
Akiongea na baadhi ya wadau wa maendseleo wa kujitolea kutoka Marekani kijijni Kitunda
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikagua chanzo cha maji ya Minispaa ya Lindi kilichopo Kitunda kata ya Msinjahili manispaa hiyo leo mchana kwenye siku ya pili ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Lindi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
Viongozi wa mkoa wa Iringa wakimpa maelezo Rais Jakaya Kikwete baada ya kuwasili katika mkoa huo kwa ziara ya kikazi
Rais Jakaya Kikwete akiongea na mmoja kati ya watoto wa mkoani Lindi waliofika kumpokea
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja kati ya wadau wa maendeleo wa kigeni
Habari na picha na Abdulaziz Video
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaJakaya Mrisho Kikwete amewaambia viongozi kuwa kazi yao kubwa ni kusikiliza nakutafuta majawabu ya matatizo na kero za wananchi badala ya kuendekeza umangimembe kwa kujisikia katika maofisi yao.
Rais amesema kuwa kila kiongozi kwa ngazi yake anao wajibuwa kukabiliana na kumaliza matatizo na kero za wananchi walio chini yake badala ya kusubiri uongozi wa juu yake kutafuta ufumbuzi na majawabu ya matatizo ya wananchi wake.
Rais Kikwete ametoa kauli yake jioni ya jana, Jumamosi,Agosti 20, 2011 wakati alipozungumza na viongozi wa Mkoa wa Lindi baada ya kuwaamekula futari nao mjini Lindi na kutumia nafasi hiyo kutaka kujua hali yatatizo la maji linaloukabili mji wa Lindi.
Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi yasiku mbili Mkoani Lindi alitoa kauli hizo kuhusu uongozi baada ya kuwaamekutana na viongozi wa Mkoa wa Lindi kutaka kujua hali ya upatikanaji majikatika mji wa Lindi na jitihada za uongozi wa Mkoa huo kukabiliana na tatizohilo.
Rais Kikwete ameelezea umuhimu wa viongozi kutimizawajibu wao baada ya kuwa amejulishwa kuwa moja ya sababu ya kukosekana maji yakutosha katika Mji wa Lindi ni kukosekana kwa kiasi cha sh. 25,000,000 kwaajili ya kununulia mafuta ya dezeli kusukuma mitambo ya umeme kwenye chanzo chaumeme cha Kijiji cha Kitunda.
Rais Kikwete alihoji inakuwaje uongozi mzima wa Mkoa waLindi ukiwamo wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Maji la Mji waLindi (LUWASA), Halmashauri ya Mji wa Lindi na ule wa Mkoa wanashindwa kutafutakiasi cha sh 25,000,000 ili kuwapatia wananchi maji.
Rais Kikwete katika kuhakikisha kuwa fedha hizohaziendelei kuwa kikwazo cha upatikanaji wa maji, aliagiza ngazi mbali mbali zaMkoa wa Lindi kukutana kesho, Jumatatu, Agosti 22, 2011, kuhakikisha kuwa dizeli inapatikana kuwezesha mitambo ya Kitunda kufanya kazi.
Ili kufuatilia kujua hali halisi ya upatikanaji maji,leo, Jumapili, Agosti 21, 2011, ametembelea chanzo cha maji cha Mji wa Lindikilichopo katika Kijiji cha Kitunda, Kata ya Msinjahili, Halmashauri ya Lindi ambako alielezwa hali ya upatikanaji maji kutoka katika chanzo hicho na kujionea hali halisi ya mitambo.
Kwenye chanzo hicho cha maji cha Kitunda, Rais Kikweteameonyeshwa mashine mbili za kusukumia maji, akakagua visima viwili vikubwa ambako yanavutwa maji na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
Rais Kikwete ameelezwa kuwa hali ya upatikanaji majikatika Mji wa Lindi siyo nzuri kwa sababu hadi Julai mwaka huu ni kiasi cha lita 550,000 tu za maji zilizokuwa zinawafikia wakazi 92,000 wa Mji waLindi kwa siku ambayo ni sawa na asilimia 11 tu ya mahitaji ya maji ya mji huo.
Rais Kikwete ameelezwa kuwa Mji wa Lindi unahitaji kiasi cha lita 3,000,000 za maji kwa siku.
Wakati akizungumza na wananchi wa Kitunda, Rais Kikwete amewaelekeza viongozi wa Mkoa wa Lindi kuhakikisha kuwa wananchi wa kijiji hicho cha Kitunda piawanapata maji kutokana na chanzo hicho cha maji.
Rais ametoa agizo hilo baada ya kulalamikiwa nawananchi kuwa pamoja na kwamba maji yanatoka kwenye kijiji hicho, bado wananchiwa kijiji hicho hawapati maji kutokana na chanzo hicho.
kwa hisani ya michuzi blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment