Rais Dk. Jakaya Kikwete akioneshwa na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim fulana ya Vodacom yenye logo na rangi mpya za kampuni hiyo tangu ilipobadilika kutoka buluu kuwa nyekundu Aprili Mwaka huu wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maoensho ya sekta ya mawasiliano yanayofanyika sanjari na mkutano wa mwaka wa wadau wa mawasiliano ya simu barani Afrika jijini Dar es salaam jana ambao Vodacom ni mdhamini. |
Mkuu wa Huduma za kifedha wa kampuni ya Vodacom Jacques Voogtz akiwasilisha mada juu ya njia za kusaidia maendeleo vijijini kupitia teknolojia za mawasiliano ya simu katika mkutano wa mwaka wa taasisi ya mawasiliano ya Jumuiya ya Madola - CTO unaofanyika jijini Dar es salaam. huduma ya m-pesa imekuwa mfano mzuri wa ukombozi wa kimawasiliano katika nyanja ya kifedha kwa wananchi vijijini hapa nchini. |
No comments:
Post a Comment