Mheshimiwa Januari Makamba mbunge wa bumbuli na Mwenyekiti wa kamati Nishati na Madini akichangia hoja jana Bungeni
.Mheshimiwa Anne Kilano malecela akichangia jambo Bungeni Dodoma Jana.
Mh.William Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini akiwasili Bungeni jana kuwasilisha upya makadirio na matumizi ya Wizara yake
Bunge limepitisha upya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini jana, iliyowasilishwa upya na Waziri wa Wizara hiyo Mh William Ngeleja ambaye alieleza nia thabiti ya Serikali kutokomeza kabisa tatizo la umeme Tanzania
Waziri Ngeleja aliliambia Bunge Kwamba kampuni ya Symbion Power na Shirika la hifadhi ya Taifa (NSSF) wamepewa zabuni ya kuingiza mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura
Symbion wamepewa zabuni ya kuzalisha umeme wa megawati 205, wakati NSSF wataingiza mitambo ya umeme ya kuzalisha megawati 150 ilikupunguza tatizo la mgawo wa umeme nchini.
No comments:
Post a Comment