 |
Wawakilishi wa vijana wa Tanzania katika Bunge
la Vijana wakipozi kwa picha katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini
Uingereza baada ya kuwasili nchini humo kwa ajili ya kuwakilisha vijana katika
Bunge hilo. |
Ubalozi wa Tanzania
Nchini Uingereza Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wamewateua Linda Kapinga na Lucy Minde kutuwakilisha katika mkutano wa
nne wa Commonwealth Youth Parliament ( Bunge la Vijana) ulioanza tarehe 6-10
Septemba 2011 jijini London.
 |
Wawakilishi hao wakiwa katika
mahojiano. |
Mkutano huo Umeandaliwa na Commonwealth
Parliamentary Association tawi la Uingereza ikishirikishwa na Sekretarieti ya
CPA ambayo ni Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katibu wake ni Mwafrika wa
kwanza kuteuliwa na Pia ni Mtanzania mwenzetu Dr William Shija.
 |
Pozi la picha Ubalozini
hapo.
|
No comments:
Post a Comment