Na Mwandishi wa Jeshi la
Polisi-Kagera
Polisi mkoani Kagera wamemuua kwa kumpiga risasi
mmoja ya wachimba madini wadogo waliokuwa wakijaribu kumchoma moto mwenzao mmoja
aitwaye Samwel Marwa (28), Mkazi wa Kijiji cha Runzewe, Wilaya ya Bukombe,
Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kuwaibia madini
yao.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Salewi
amesema kuwa katika harakati za kumuokoa kijana huyo pia Askari Polisi wawili
wamejeruhiwa kwa kushambuliwa kwa mawe na wachimbaji hao wa madini wakati
walipokuwa wakimuokoa mmoja ya wachimbaji hao aliyekuwa akichomwa moto kwa
tuhuma za wizi wa madini.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera SACP Henry
Salewi, amewataja Askari waliojeruhiwa kuwa walifanikiwa kumuokoa kijana huyo,
lakini Askari wawili F. 5609 D/CPL. Daniel Wangiboma na G. 3568 PC Ntimbula
Bakari walijeruhiwa kwa mawe vichwani na wamekimbizwa katika Hospitali ya wilaya
ya Biharamulo kwa matibabu.
Amesema siku ya tukio hilo jana Polisi wa Kituo
kidogo cha Mavota kwa kushirikiana na Askari Polisi wa Operesheni Wilayani
Biharamulo, walimuua mtu huyo ambaye hajafahamika jina lake wakati wakiwa katika
harakati za kumuokoa kijana huyo.
Kamanda Salewi amesema kuwa, marehemu ambaye
hajafahamika jila lake, alikuwa ni miongoni mwa kundi la wachimbaji waliokuwa
wakimshikilia kijana huyo na kuwashambulia Polisi kwa kuwapiga kwa mawe ili
kutomuokoa kijana waliodai amewaibiua madidi yao.
Kamanda Salewi amemtaja kijana aliyetunusurika
kuchomwa moto kutokana na wizo huo ambaye pia bado anahojiwa na Polisi kuwa ni
Samwel Marwa (28).
ambaye alikuwa
amekamatwa na kundi la wachimbaji wadogo wadogo wapatao 100 kwa nia ya kumchoma
moto kwa madai kwamba Samwel alikuwa amewapora dhahabu
zao.
Amesema mara baada ya kuona maisha ya kijana huyo
yalikuwa hatarini, baadhi ya wananchi walikimbia katika kituo kidogo cha Polisi
cha Mavota Wilayani Biharamulo ambapo kwa kushirikiana na askari Polisi walioko
kwenye Operation maalumu eneo la Mgodi wa Madini madini ya dhahabu wa Tulawaka
unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick, walikimbia kwenda kuokoa maisha ya kijana
huyo.
Amesema kuwa walipokaribia kwenye kundi la watu
hao, Polisi walianza kushambuliwa kwa mawe na kujaribu kufyatua risasi hewani
bila ya mafanikio na ndipo walipompiga mmoja na kuanguka na wengine kukimbia na
kufanikiwa kumuokoa kijana huyo.
Askari hao pia wamefanikiwa kupata mafuta lita
tatu aina ya Petrol ambayo ilikuwa itumike kwa kumchomea moto kijana huyo.
Amesema
kuwa katika tukio hilo watu wanne walikamatwa kuhusiaka na jaribio hilo la
mauaji na amewataja waliokamatwa kuwa ni Jejo Motopasi(26) Simon
Motopasi(22) na James Vicent(20) wote wakazi wa Kiji cha Runzewe Wilaya ya
Bukombe na Vicent Idian(25), Mkazi wa Kijiji cha Mavota Wilayani
Biharamulo.
No comments:
Post a Comment