Baadhi ya Washiriki wa Mbio za Mashua,
zijulikanazo kama TANZACAT wakipunga Mikono kuashirika kuanza kwa mbio hizo
zilizozinduliwa rasmi jana katika Klabu ya Yatch jijini na kudhaminiwa na
kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
Baadhi ya Washiriki wa Mbio za Mashua,
Zijulikanazo kama TANZACAT wakianza Mbio hizo jana katika Ufukwe wa bahari ya
Hindi eneo la Klabu ya Yatch jijini Dar es Salaam ambapo Mashindano hayo
yanayochukua siku saba yanadhaminiwa na kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom
Tanzania.
Mwenyekiti wa mbio za mashua Nicholus
Zervos akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mbio hizo zilizoshirikisha
mataifa 16 na kuwashukuru wadhamini wakuu Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
Tanzania.
Mshiriki wa Mbio za Mashua zijulikanazo
kama TANZACAT, Belia Klaassen, aliyewahi kushiriki mbio hizo kwa miaka kumi
nchini Tanzania akielezea namna anavyofurahia kushiriki mashindano hayo tena
na jinsi yalivyoboreshwa zaidi jana jijini Dar es
salaam
Mmoja wa washiriki wa mbio za mashua
zijulikanazo kama TANZANCAT Evelyne Geubbels (kulia) akieleza namna mbio hizo za
ufunguzi zinazodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania
zilivyofana katika Klabu ya Yatch jijini, kushoto ni mshiriki mwenzake Jerome
Vant Pad Bosch.
Mwenyekiti wa mbio za mashua Nicholus
Zervos (wa pili kulia)akiwa na baadhi ya washiriki wa mbio hizo mara baada ya
ufunguzi wa mbio hizo jana jijini ambapo zitaendelea kwa muda wa siku saba na
kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
Tanzania
No comments:
Post a Comment