Kikao malum kuhusu Libya,
ambacho mwenyeji wake ni Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Waziri Mkuu wa
Uingereza David Cameron, kinafanyika punde mjini Paris.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton
atahudhuria huku China na Urusi, wakilitambua Baraza la Mpito la Libya (NTC)
kama serikali halali ya Libya. Baraza hilo la NTC litaomba msaada wa ulinzi,
kuijenga upya Libya na kuandaa kwa ajili ya demokrasia. Lakini bado
halijamkamata Kanali Gaddafi ambaye mtoto wake Saif al-Islam ameapata tena
kupigana mpaka kufa.
Mwandishi wa BBC Jon Leyne, akiwa Benghazi, anasema
ingawa mkutano wa Paris utakuwa mfupi na uwakilishi, utazipa serikali ambazo
zinaliunga mkono NTC nafasi nyingine ya kuonyesha kuwa lina uwezo katika uwanja
wa kimataifa. Anasema mkutano utazingatia mipango ya mpito kuelekea demokrasia,
kwa ajilio ya kuijenga Libya upya na mambo kama kuliwezesha kimafunzo jeshi la
polisi.
Baraza la NTC, mwandishi wa BBC anasema
litashinikiza kuachiliwa zaidi kwa mali ya Libya iliyotiwa tanji lakini
litasisitiza kuwa halitaki NATO ipunguze msaada wake wakati ikimalizia kuwaondoa
masalia ya vikosi vya Kanali Gaddafi. Libya, na utajiri wake mkubwa wa mapato
yatokanayo na mafuta huku ikiwa na idadi ndogo, si nchi ya kikapuni. Itahitaji
mdsaada mkubwa wa kuijenga upya. Hata hivyo kuna wengi walio tayari
kuisadia.
Uingereza na Ufaransa, ambazo zilishinikiza kuwa na
harakati za kijeshi za anga ambazo ziliongozwa na Muungano wa NATO, wana nia ya
kuongoza jukumu la kuijenga upya Libya. Katika mkodno huo, yupo mshirika wa muda
mrefu wa Libya barani Ulaya-Italia
Source: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment