Saturday, September 17, 2011

Ajali ya meli yapandisha bei ya samaki Dar!

BEI ya samaki katika jiji la Dar es Salaam imepanda kwa kiwango cha juu kufuatia ajali ya meli ya Mv Spice Islender.
Uchunguzi uliofanywa, jana, umebaini kuwa upatikanaji wa samaki umekuwa mgumu, kutokana na wavuvi wengi kuwa wale wanaotoka kisiwani Pemba ambao walikuwa wakiombolezo vifo vya ndugu zao waliopoteza maisha katika ajali ya meli hiyo.
Mmoja wa wafanyabiashara ya samaki katika soko la Feri, Seleman Juma, alisema upungufu huo wa samaki umewalazimu kupandisha bei kwa wale wachache wanaopatikana.
“Unajua wavuvi wengi wanatoka Pemba. Na katika ajali hii, wameathirika sana kwa sababu ndugu zao wengi wamefariki,” alisema Seleman.
Seleman alisema bei ya samaki aina ya nguru imepanda kutoka sh 40,000 hadi 100,000. Samaki aina ya Jodari kwa sasa ni 100,000 badala ya 70,000 ya zamani.
Katibu wa soko la Mbagala Rangi Tatu, Frank Mapuli, amekiri upungufu wa samaki uliochangiwa na ajali ya meli.
Husna Hamad, mfanyabiashara ya samaki katika soko la Magomeni, alisema samaki wameadimika na kusababisha bei kupanda.

Source, Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

hostgator coupon code