Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Jengo la Mihadhara na kuchangisha fedha za ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE jijini Dar es Salaam leo. Kusho ni mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDSM, Prof. Yunus Mgaya na (kulia) ni Mkuu wa Chuo hicho Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua Ukumbi wa miku cha mihadhara kilichopo katika jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, baada ya uzinduzi uliofanyika Chuoni hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia picha yake iliyoandaliwa maalu kwa ajili ya kupigwa mnada katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari ya Chang’ombe. Picha hiyo ilinunuliwa kwa Sh, milioni 3, 800.000.
Makamu wa Rais, akimpongeza mmoja kati ya watu waliojitolea kuchangia ujenzi huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Diamond Security, Haroun Mdoe, aliyechangia Sh. milioni 1.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mchango wa sh. 60,000 uliotplewa na watoto wa Shule ya awali ya Duce kutoka kwa mtoto, Edna Mayungi, wakati wa zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya sekondari Chang’ombe lililofanyika wakati wa uzindu wa Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE leo Septemba 13 jijini Dar es Salaam. Katika zoezi hilo zilipatikana jumla ya Sh. Milioni 158 kwa njia ya ‘Cash’ Ahadi na Mnada. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Terezya Huvisa (kushoto) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana, baada ya kuzindua rasmi Jengo la Mihadhara la chuo hicho.
Watoto wa Shule ya awali ya DUCE, wakiimba ngonjela mbele ya mgeni rasmi, wakati wa uzinduzi huo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji na maofisa wa Chuo hicho baada ya uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment