Katibu wa Uchumi na Fedha waCCM Taifa, Mwigulu Nchemba, akihutubia wananchi wa kijiji cha Nkinga leo mchana katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga. Akihutubia wananchi wa Nkinga, Nchemba aliwataka wakazi hao kumchagua mgombea wa CCM, Dr Dalali Kafumu, kuwa mbunge wao chama atokacho CCM, ndio chama pekee chenye sera zinazotekelezeka. Aliwaasa wananchi wa Nkinga na Igunga kwa ujumla kutochagua wagombea wa vyama vya upinzania kwani vyama hivyo vipo kwa maslahi ya viongozi wake na sio kwa maslahi ya wananchi. "Ndugu zangu wana Nkinga, msithubutu kuchagua vyama vya upinzani, chagueni CCM kwa ajili ya mendeleo yenu. Chama cha CCM, ndicho chama pekee chenye sera zinazotekelezeka. Hawa wenzetu wapinzani hawa, hawana lolote. Vyama vyao ni porojo tupu. Vipo kwa maslahi ya viongozi tu na sio kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania." Picha zote na Victor Makinda |
No comments:
Post a Comment