Sunday, September 11, 2011

Makamu Wa Rais Awafariji Waliopotelewa Na Ndugu

1. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wakazi viongozi na wakazi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuwafariji wakazi hao waliopatwa na matatizo pamoja na kukagua shughuli za uokoaji, jana Septemba 11, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua maeneo yaliyokuwa yakitumika kupokelea na kuhifadhi miili ya watu waliokufa katika ajali ya meli ya Spice, pamoja na majeruhi waliokuwa wakipitishwa katika eneo hilo la Ufukwe wa Bahari ya Hindi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja jana Septemba 11, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

hostgator coupon code