Sunday, October 2, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU YA WIZARA YA AFYA YAFUNGWA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin.
Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin akizungumza wakati wa kufungwa kwa maadhimisho hayo ambapo ameipongeza Tanzania kwa Mafanikio iliyofikia katika utoaji huduma za Afya katika Kipindi cha Miaka 50 iliyopita haswa katika kupunguza vifo vya watoto wadogo ambapo Tanzania kwa sasa imefanikiwa kupunguza vifo 110.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Idara mbalimbali za Wizara ya Afya wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara hiyo. Mhe. Lucy Nkya
Mgeni rasmi akiongea na baadhi ya Wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma za Upimaji na Matibabu ya Masikio, Koo na Pua.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Burudani ya Muziki kutoka kwa Mjomba Bendi katika kunogesha sherehe za kufungwa kwa maadhimisho hayo.
Meneja Habari na Ushauri wa Taasisi ya John Hopkins Centre For Communication Programme Tanzania Fauziyat Abood akitoa ufafanuzi wa Shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo kwa mgeni rasmi alipotembelea katika banda hilo.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara na Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini.

No comments:

Post a Comment

hostgator coupon code