Thursday, September 29, 2011

SPIKA WA BUNGE MAMA ANNA MAKINDA AMTEMBELEA DK MWANDOSYA HOSPITALINI NCHINI INDIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda akimjulia hali Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya alipomtembelea katika hospitali ya Apollo nchini India ambako Profesa Mwandosya amelazwa kwa matibabu. Hali yake inaendelea vyema
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Seif Shariff Hamad akiwa katika mazungumzo na Prof. Mark Mwandosya na Bwana Rodhey Mohan, Meneja Mkuu wa Hospitali ya Apollo alipofika kumjulia hali Prof Mwandosya ambaye amelazwa hapo kwa matibabu baada ya kuhitimisha ziara yake India iliyomchukua katika majimbo ya Andhara Pradesh, Kerala na Karnataka.
 
Kutoka kushoto ni Mhe. Mohamed Aboud (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili, Zanzibar), Mama Lucy Mwandosya, Bw. Radhey Mohan, Meneja Mkuu wa Hospitali ya Apollo, Mhe. SEIF Shariff Hamad na Prof. Mwandosya

AIRTEL TANZANIA NA ENGEN PETROLEUM ZACHANGIA KUFANIKISHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani, Kamishana Mohamed Mpinga wakionesha stika hizo kwa waandishi wa habari
 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaban Kayungilo na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani, Kamishana Mohamed Mpinga wakionesha stika hizo kwa waandishi wa habari
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta ENGEN kwa pamoja wameungana na serikali ya jamuhuri ya Tanzania kwa kupitia baraza la taifa la usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti namba ya ajali za barabarani nchini.
Leo tumekutana hapa kutangaza wiki ya nenda kwa usalama ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Bukoba. ENGEN Tanzania kampuni ya nishati ya magari nchini Tanzania na Airtel kampuni ya mawasiliano zilikubaliana kuungana na serikali kupitia Baraza la Usalama Barabarani na Jeshi la polisi kuhamasisha jamii kahusu usalama barabarani ili kupunguza ajali.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ENGEN Meneja Bidhaa Jacqueline Kisoka Kupitia SLOGAN ya mwaka huu inayosema “ Usalama barabarani unahitaji uwajibikaji wa kila mtu” ENGEN Tanzania inayofuraha kuwa sehemu ya jitihada za kuokoa maisha ya watu katika jamii yetu na imejitoa kuhamasisha jamii nzima kuzingatia usalama barabarani kama mchango wake katika huduma kwa jamii. ENGEN ni sehemu ya watumia barabara na watumia barabara wengi hutumia bidhaa za ENGEN ndio maana ni mategemeo ya ENGEN kuwa watumia barabara wote wawe salama ili iweze kuwahudumia.
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “kwa miaka 3 mfululizo Airtel kwa kushirikiana na Baraza la Usalama Barabaaarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa. Mchango wetu kwa mwaka huu ni kuchapisha stika na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 2,200 zenye ujumbe wa mwaka huu “Usalama Barabarani unahitaji juhudi za kila moja wetu” .
Matokeo ya ajali za barabarani ni moja ya masuala muhimu kiafya kitaifa. Kila mtumia barabara anahusika awe mwendesha gari, pikipiki au mtembea kwa miguu. Kila mwaka maelfu ya wanaume, wanawake na watoto hufariki kutokana na ajali za barabarani hivyo kusababisha upungufu wa nguvu kazi katika shughuli za uzalishaji kiuchumi. Hii ndio sababu Airtel imejiingiza katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha jitihada hizi”.
Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mallya aliongeza
Note:
Umuhimu wa usalama barabarani hauwezwi kupuuzwa, kila siku tunashuhudia ajali nyingi zikisababisha kupoteza maisha, wa Tanzania wengi, uharibifu wa mali nyingi zenye thamani ya mamilioni. Zaidi ya mguso wa kibinadamu utokanao na ajali za barabarani lakini pia maafa na majeraraha yatokanayo na ajali za barabarani zinaleta athari za kijamii na kiuchumi. Kwa mfano takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa watu 2,850 wanapoteza maisha kila mwaka katika ajali za barabarani. Takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kwamba watu 3,582 walipoteza maisha huku majeruhi wakiwa zaidi ya 20,000 wakati watembea kwa miguu na wapanda baiskeli wakiwa hatarini zaidi.
Mwaka 2010 katika jumla ya ajali 22,750 gharama au hasara iliyotokana na ajali za barabarani zinakadiriwa kufika bil 363. Hii ni athari kubwa kiuchumi.

Monday, September 26, 2011

Petroli, dizeli yapanda tena


BAADA ya bei ya petroli kushuka kwa wiki nne mfululizo, leo bei ya bidhaa zinazotokana na nishati hiyo zitapanda na kudumu kwa wiki mbili zijazo.Safari hii petroli katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh 2,102 kwa lita moja ikilinganishwa na Sh 2,031 kwa bei, iliyoishia jana.

Kupanda na kushuka kwa bei ya nishati hiyo ya mafuta kwa lita, ni sehemu ya utekelezaji wa kanuni ya ukokotoaji inayotumiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).

Wiki mbili zilizopita, Ewura ilitoa bei elekezi ambazo petroli ilishuka kwa Sh38.03 sawa na asilimia 1.84, dizeli Sh 45.15 sawa na asilimia 2.26 na mafuta ya taa bei ilishuka kwa Sh46.15 sawa na asilimia 2.33.

Hata hivyo, jana Ewura katika bei hizo mpya inayoanza kutumika leo imetangaza kupanda kwa bei ya rejareja ya petroli kwa Sh 70.12 sawa na asilimia 3.57 wakati dizeli imepanda kwa Sh 44.88 sawa na asilimia 2.38 na mafuta ya taa kwa Sh 33.02 sawa na asilimia 1.77.

Mkurugenzi wa Petroli wa Ewura, Mutaekulwa Mutegeki alitangaza bei hiyo jana, huku ikionyesha kuwa kwa Dar es Salaam petroli itauzwa kwa Sh 2,102, mafuta ya taa Sh1,967 na dizeli Sh1,999 kwa bei ya rejareja.

Bei ya rejareja katika miji mingine mikubwa ni Arusha ambako petrol itauzwa Sh2,186, mafuta ya taa Sh2,051 na dizeli Sh2083.

Mbeya, petroli itauzwa Sh2,209 kwa lita moja, mafuta ya taa Sh2,074 na dizeli Sh2,106, wakati Mwanza petroli itauzwa kwa Sh2,251, mafuta ya taa Sh2,116 na dizeli Sh2,149.

Sababu za kupanda

Ewura walisema sababu za kupanda kwa bei hiyo ya mafuta ni kutokana na kupanda kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia.

Ewura katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, ilifafanua kuwa petroli imepanda kwa asilimia 5.16, dizeli 2.98 na mafuta ya taa kwa asilimia 2.35.

Pia Ewura imetangaza sababu nyingine, ni kuendelea kupomoroka kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani kwa kiwango cha asilimia 0.55.

Mkurugenzi huyo wa Petroli alisema, kuporomoka kwa shilingi dhidi ya dola ambayo ni fedha ya kimataifa ya manunuzi kumefanya manunuzi ya ndani nayo kuongezeka.

Mchakato kuanzia Agosti 2

Mchakato wa marekebisho ya bei za mafuta, ulianza Agosti 2, mwaka huu ambapo Ewura ilitangaza kushusha bei ya mafuta ambayo petroli ilishuka kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ni sawa na asimilia 9.17, dizeli ilishuka kwa Sh173.49 ambayo ni sawa na asilimia 8.32 na mafuta ya taa yalishuka bei kwa Sh181.37, sawa na asilimia 8.70.

Hata hivyo, uamuzi huo uliibua mvutano kati ya wamiliki wa makampuni ya mafuta na serikali huku wamiliki hao wakitunisha msuli na kugoma kuuza nishati hiyo muhimu.

Lakini, Agosti 10 serikali ilitoa saa 24 kwa kampuni hizo za mafuta kutangaza kwanini yasichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka agizo halali la serikali.

Ewura baadaye ilitoa onyo kwa kampuni zilizogoma ikiwemo Engen, Camel Oil, huku ikimfungulia mashitaka mkurugenzi mkuu wa BP kwa kushindwa kutii amri ya kushusha bei.

Lakini, siku 11 baada ya kushusha bei na nchi kutikiswa na mgomo Ewura ilipandisha tena bei kwa kisingizio cha kuporomoka kwa shilingi na kupanda kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia.

Hata hivyo, wiki mbili zilizopita hadi kuishia jana Ewura ilitangaza kushusha bei tena ya mafuta na kutoa ahueni kwa watumiaji nchini.
Source Mwananchi

Saturday, September 24, 2011

WAATHIRIKA WA MABOMU YA GONGO LA MBOTO WAKIWA KWENYE FOLENI TAYARI KWA KUPOKEA MALIPO YA FIDIA YA NYUMBA ZAO


Baadhi ya wakazi wa Kata ya Majohe Gongolamboto wakiwa katika foleni Dar es Salaam jana ya uhakiki ili kupokea malipo ya fidia ya thamani za ndani na matengenezo ya nyumba zilizoathirika na milipuko ya mabomu iliyotokea kwenye Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) mwezi Februari mwaka huu.Picha Na Majira

Thursday, September 22, 2011

Uholanzi yatoa Sh30 bilioni kugharamia elimu nchini


Tanzania itafaidika na msaada wa Euro Milioni 15 ( zaidi ya Sh30 bilioni ) toka Serikali ya Uholanzi kugharimia mradi wa Kujenga Uwezo kwa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, unaojulikana kwa jina la Netherlands Initiative for Capacity Development in Higher Education(Niche).

Hayo yalibainishwa na meneja wa mradi huo, Ute Jansen, alipotembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro, kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao kwa chuo kikuu hicho, mradi huo unatoa ufadhili kwa Shule ya Biashara na kuboresha mafunzo ya utawala wa Serikali za Mitaa.

Jansen, alisema ana matumaini makubwa sana kuwa mradi huu utakapokamilika, utaboresha sana zile sekta zilizoainishwa kwenye mradi huu ambazo ni kujenga uwezo katika kutoa elimu kuhusu afya, sekta binafsi na Serikali za Mitaa.

Kwa upande wake, msimamizi wa mradi huo Tanzania, kupitia Shirika la NUFFIC, Johanna Van Nieuwenhuizen, alisema Uholanzi imeridhishwa na jinsi Tanzania inavyoitumia misaada toka nchini mwake, hivyo kujihakikishia fursa zaidi za kusaidiwa katika miradi mbalimbali.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Mugishi Mgasa, aliyemwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo, aliishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kufadhili mradi huo na kueleza kuwa ufadhili huo una maana kubwa sana kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe, kwa sababu utapanua uwezo wa chuo hicho katika kutoa Mafunzo ya Biashara na Utawala wa Serikali za Mitaa.

Naye Mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Joseph Kimeme, alisema ufadhili huo, utawafanya wanafunzi wanaomaliza Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, sio tu kuhitimu kwa elimu yenye ubora wa hali ya juu, bali pia watajengewa uwezo wa kujiajiri kwenye biashara zao kufuatia mahitaji ya soko.

Rais Jakaya Kikwete Apokea Tuzo Mbili Maalum Kwa Mchango Wake Mkubwa Katika Afya ya Mama Mjamzito na Watoto,Akutana Na Viongozi Mbalimbali

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihudhuria mkutano wa 'Social Good Summit' anapokea tuzo kutoka United Nations Foundartion for his work in Martenal Health and Social Media Commitment kutoka kwa Makamu wa Rais wa Public Policy of United Nations Foundation Mr. Peter Yeo katika sherehe fupi iliyofanyika jijini New York .
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki- Moon kwenye Makao Makuu ya Umoja Mataifa jijini New York nchini Marekani.Kwa Picha

Sakata La Mkuu Wa Wilaya ya Igunga; Wanazuoni Wa Kiislamu Waivaa CHADEMA


Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewekwa kitanzini baada ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania (HAY-AT) kutoa muda wa
siku tatu kwa viongozi wake wa taifa kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitara yake na kumdhalilisha.


Pia umoja huo umeonya kuwa iwapo CHADEMA hawatafanya hivyo wataandaa maandamano nchi nzima kutangaza chama hicho kuwa adui mkubwa wa dini hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bw. Sherally Sherally alisema kitendo kilichofanywa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA ni udhalilishaji kwa mwanamke wa kiislamu hivyo ni lazima viongozi wake wa juu walaani waliohusika na kuomba radhi.

Tayari watu watatu wakiwamo wabunge wawili wamefikishwa mahakamani mkoani Tabora wakituhumiwa kwa kumshambulia Bi. Kimario na kumwibia simu yake yenye thamani ya sh 400,000. Watuhumiwa hao waliachiwa juzi kwa dhamana hadi Agosti 10, mwaka huu.

Bw. Sherally alisema iwapo chama hicho kitapuuza agizo hilo kwa muda waliowapa umoja huo utapita nchi nzima kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo dhidi ya mwanamke.

"Tunalaani na kupinga kwa ukali kabisa kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa ni wafuasi na viongozi wa CHADEMA kumvua hijabu Bi. Kimario na kumuacha bila stara huko Igunga Septemba 15," alisema Bw. Sherally na kuongeza:

"Kitendo hiki kumvua hijabu Bi. Kimario, kumsukasuka na kumtolea maneno yasiyofaa ni kitendo kiovu sana mbele ya Mwenyezi Mungu, Waislam na Watanzania wote wapenda haki na amani na wanaojiheshimu," alisema.
Katika hatua nyingine Bw. Sherally alisema wamesikitishwa na kushitushwa na kukaa kimya kwa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na wanawake kwa kutolaani kitendo hicho cha mwanamke mwenzao kudhalilishwa kijinsia."Kuendelea kukaa kwao kimya kutatulazimisha kuwaona kuwa wanaafiki na ndumilakuwili," alisema.Chanzo Gazeti Majira.

Wednesday, September 21, 2011

Man city yaweka wazi mpango wake wakujenga "Training Academy Complex"

 
Man city imeweka wazi mpango wake wa kujenga uwanja mpya ambao utatumika kama chuo cha michezo kwa vijana hivi karibuni, Man city ilinunuliwa na bilionea wa Abu Dhabi Sheikh Mansour Bin Zayed Al Nahyan August 2008 na toka hapo amekuwa akiwekeza hela nyingi sana katika kuiinua timu hiyo.
Academy hiyo itakayo jengwa karibu na uwanja wao wa Etihad Stadium, itakuwa na viwanja 15 vya mpira na uwanja utaochukua watu 70,000 wakiwa wamekaa, pia complex hiyo itakuwa na vyumba vya kulala kwa timu 40 kwa wakati mmoja. stay tune for more detail

Tuesday, September 20, 2011

(VOTE) MT. Kilimanjaro nominated as candidate for the new seven natural wonders of the world


Mount Kilimanjaro

                                                                     Mt. Kilimanjaro

Tanzania Tourist Board wishes to inform the public that Mount Kilimanjaro has been nominated as a candidate for the seven natural wonders of the world, in a competition organised by an organisation known as Seven Natural Wonders in which tourist attractions from all over the world are voted to nominated as The Seven Natural wonders of The World.
Tanzania will gain much publicity from being listed in the new list of Seven Natural wonders of the World and will be able to use this opportunity to promote Mt. Kilimanjaro as being in Tanzania.
Out of the 28 contestants which have made it to this stage, only two nominations are from Africa, these being Mt. Kilimanjaro (Tanzania) and Table Mountain (South Africa). There is fierce competition between the two African destinations.
Voting trends have shown that most people who are voting for Mount Kilimanjaro are those residing outside the country and that very few Tanzanian residents are voting for Mt. Kilimanjaro unlike the case for Table Mountain where large numbers of South Africans are taking participation in voting for Table Mountain.
We (TTB) would like to urge Tanzanians (in and out of Tanzania), friends and patrons worldwide to vote for Mount Kilimanjaro so that it becomes one of the New Seven Natural Wonders Of The World.
Votes are being collected at the following website: www.new7wonders.com
Note that the competition is open until November 11th, 2011.

One of the Seven Natural Wonders of Africa (Ngorongoro Crater)




Black Rhinos Ngorongoro Crater

Ngorongoro Crater is the world's largest unbroken caldera. Often referred to as "Africa's Garden of Eden," the crater is home to over 30,000 animals including elephants, lions, cheetahs, wildebeests, buffaloes, and the rare black rhinos. View Wildlife of Ngorongoro Crater to learn more about the wildlife and View Birds of Ngorongoro Crater
to discover some of the many species that are found in the area.
Ngorongoro Crater was created from a volcano that exploded creating the caldera wilderness haven. The crater is 12 miles (19 km) across and consumes 102 square miles (264 sq km) of wilderness. The rim of the crater rises just over 2,000 feet (610 m) above the caldera floor reaching an elevation of 7,500 feet (2,286 m).

WABUNGE CHADEMA WAACHIWA TOKA RUMANDE WAPOKELEWA KWA SHANGWE NA VIFIJO


Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kueapokea wabunge wao wa CHADEMA mara baaada ya kutolewa Rumande




Wanachama wa CHADEMA mjini Igunga, walijawa na furaha kubwa wakati wakiwa wanawapokea wabunge wao waliokamatwa hivi karibuni na kuwekwa rumande mjini Igunga na baadae kuhamishiwa kituo cha polisi mkoani Tabora kwa kosa la kumvamia na kumgasi mkuu wa Wilaya ya Igunga Fatuma Kimario. Wabunge hao ni Sylivester Kasulumbai, mbunge wa Maswa Mashariki, Suzani Kiwanga, ambae ni mbunge wa viti maalumu. Mwingine ni kada wa chama hicho. Kwa pamoja wamepata dhamana na kesi yao itatajwa tarehe 12.10.2011. Pichani wakiwa katika maandamano jioni hii mjini Igunga. Picha na Victor Makinda.

Saturday, September 17, 2011

Vijana washtukia mtego wa CCM

VIJANA wanaharakati wa mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameonyesha kushtushwa na mkakati wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 sasa kwa kuwarubuni vijana kwa kuanzisha Benki ya Vijana nchini.
Walidai kuwa kuanzishwa kwa benki hiyo si suluhisho la tatizo la ajira kwa vijana nchini, kutokana na mfumo wa uanzishwaji wake ulivyo kwa sasa ambao una lengo la kuwavuta vijana kisiasa zaidi.
Wakizungumza katika kipindi cha malumbano ya hoja kilichorushwa na kituo cha televisheni cha juzi, walisema wazo la kuwa na benki ya vijana ni zuri na linaungwa mkono na vijana wote, ila mfumo wa uanzishwaji wake ndio unawatia hofu.
Walisema kutokana na hali ya kisiasa ilivyo na vijana wengi kupoteza imani na CCM, ni wazi chama hicho kimekuja na wazo hilo la kuanzisha benki kama njia ya kujijenga kisiasa.
Ally Salum Ally kutoka Pemba alisema kuwa benki hiyo ilipaswa kuanzishwa baada ya kuunda chombo cha vijana ambacho kitakuwa huru pasipo kufungamana na chama chochote cha kisiasa.
Sarah Kyando kutoka mkoa wa Mbeya alisema kuwa serikali ya CCM imeendelea kuja na mikakati mbalimbali ambayo mwisho wa siku imejikuta ikizidi kuchafuka zaidi kutokana kutokuwa na utekelezaji.
Mwakilishi wa benki hiyo, Christopher Ngubiagai, akijibu maswali ya wanaharakati hao alisema kuwa benki hiyo pamoja na kuanzishwa na UVCCM, haitabagua vijana wa vyama vingine.

Source Tanzania Daima

Ajali ya meli yapandisha bei ya samaki Dar!

BEI ya samaki katika jiji la Dar es Salaam imepanda kwa kiwango cha juu kufuatia ajali ya meli ya Mv Spice Islender.
Uchunguzi uliofanywa, jana, umebaini kuwa upatikanaji wa samaki umekuwa mgumu, kutokana na wavuvi wengi kuwa wale wanaotoka kisiwani Pemba ambao walikuwa wakiombolezo vifo vya ndugu zao waliopoteza maisha katika ajali ya meli hiyo.
Mmoja wa wafanyabiashara ya samaki katika soko la Feri, Seleman Juma, alisema upungufu huo wa samaki umewalazimu kupandisha bei kwa wale wachache wanaopatikana.
“Unajua wavuvi wengi wanatoka Pemba. Na katika ajali hii, wameathirika sana kwa sababu ndugu zao wengi wamefariki,” alisema Seleman.
Seleman alisema bei ya samaki aina ya nguru imepanda kutoka sh 40,000 hadi 100,000. Samaki aina ya Jodari kwa sasa ni 100,000 badala ya 70,000 ya zamani.
Katibu wa soko la Mbagala Rangi Tatu, Frank Mapuli, amekiri upungufu wa samaki uliochangiwa na ajali ya meli.
Husna Hamad, mfanyabiashara ya samaki katika soko la Magomeni, alisema samaki wameadimika na kusababisha bei kupanda.

Source, Tanzania Daima

Serikali yasema "DC amedhalilishwa"....

SERIKALI imesikitishwa na udhalilishaji uliofanywa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatma Kimario juzi.

Imesema kwa kuwa nchi inafuata utawala wa sheria, inaviachia vyombo vya Dola vifanye uchunguzi wake.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, alipozungumza na gazeti hili akiwa Newala mkoani
Mtwara.

“Serikali imesikitishwa na udhalilishaji uliofanywa kwa DC wa Igunga. Nchi ina taratibu, kanuni na sheria kwa hiyo unaviachia vyombo vya Dola kufanya kazi yake. “Lakini tumesikitishwa na tukio lile kwa sababu DC alikuwa tayari kusema nao, alikuwa eneo lake la utawala akifanya kazi. Kwa nini wamkamate na kumtoa nje kwa udhalilishaji ule,” alisema Mkuchika.

Alisema haikuwa vyema kwa wahusika kufanya udhalilishaji huo hasa baada ya Mkuu huyo wa wilaya kuwa tayari kuzungumza nao; hivyo wangeweza kuzungumza naye ofisini katika mazingira ya ustaarabu.

DC Kimario alifanyiwa vurugu na vijana wa Chadema juzi akiwa katika shughuli zake za kikazi.

Vijana hao walidai DC alikuwa akifanya kampeni za kisiasa katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Igunga utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu.

Katika taarifa yake jana, Polisi ilisema DC huyo amefanyiwa shambulio la kudhalilisha kinyume cha maadili, ikiwemo kuvuliwa vazi lake la hijab ambalo humsitiri mwanamke wa Kiislamu hasa kichwani. Akizungumza jana wilayani Igunga, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini wa Polisi, Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Isaya Mngulu, alisema mbali na kuvuliwa hijab, pia DC alidai alivuliwa viatu na kukatiwa mkufu.

"Pia simu yake ya mkononi aina ya Samsung ilipotea na alitukanwa matusi ya nguoni ya kumdhalilisha …(hatuwezi kuyaandika hapa)," alisema Mngulu akielezea madai hayo ya DC Kimario.

Alisema wakati Mkuu huyo wa Wilaya akifanyiwa vitendo hivyo na vijana hao wa Chadema, Ofisa Tawala wa Wilaya ya Igunga, Sunera Manoti, alikwenda Polisi kutoa taarifa.

Hata hivyo, baada ya Polisi kupata taarifa hiyo, kwa mujibu wa Mngulu, walikwenda eneo la tukio na kukuta hali ni shwari na kuanza upelelezi baada ya majalada ya tuhuma; la kwanza la DC akilalamika kufanyiwa shambulio la aibu na la pili la Chadema wakilalamikia kuingiliwa katika mkutano wa kampeni.

Kwa mujibu wa taarifa za Chadema, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga, Mbunge wa Maswa Mashariki, Kasulumba Sylvester pamoja na shabiki wao ambaye jina lake halikupatikana waliitwa Polisi na kuhojiwa saa moja na kuachiwa kwa dhamana.

Madai ya Chadema Awali, kabla ya Polisi kuzungumzia hilo, Chadema iliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelezea makosa 15 ya DC huyo, likiwemo la kuitisha mkutano waliodai kuwa ni wa hadhara na kinyume cha sheria.

Akifafanua madai hayo, Mkurugenzi wa Chadema wa Oganaizesheni na Mafunzo, Benson Singo, alidai kuwa mtu ye yote akitaka kufanya mkutano, lazima atoe taarifa kwa Polisi na kwa kuwa polisi walikuwa wakifahamu kuwepo kwa mkutano wa Chadema, wasingemruhusu DC kufanya wa kwake.

Hata hivyo, Mngulu alisema DC Kimario alikuwa katika kikao cha ndani na sio mkutano wa hadhara kama Chadema walivyodai, ambacho kisingehitilafiana na mkutano huo wa Chadema, lakini hata muda wa tukio la kushambuliwa Mkuu huyo wa Wilaya na mkutano wa Chadema vilikuwa tofauti.
  for more detail visit http://www.habarileo.co.tz/

Watu wanne akiwemo na Nahodha wastakiwa kwa kuzama kwa Meli Zanzibar

WATU wanne akiwemo nahodha wa meli ya mv Spice Islander wameshitakiwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar wakihusishwa na kuzama kwa meli hiyo Jumamosi alfajiri na kuua watu zaidi ya 200.
Nahodha wa meli hiyo, Said Abdallah Kinyanyite (58), msaidizi wake Abdallah Mohamed Ali (30), Ofisa Usalama wa Bandari ya Zanzibar, Simai Nyange Simai (27), na ofisa kutoka katika kampuni inayomiliki meli hiyo, Yussuf Suleiman Jussa (47), ndio waliopanda kizimbani.

Wanashitakiwa kwa makosa ya uzembe chini ya Kifungu 236 cha Sheria Namba 6 ya Zanzibar ya mwaka 2004. Hata hivyo, nahodha wa meli hiyo, hakuwepo mahakamani mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi ambaye pia alikataa kutoa dhamana kwa washitakiwa wengine kama alivyoombwa na wakili wa utetezi Hamid Mbwezeleni.

“Hii ni kesi nyeti, nasita kukimbilia katika kutoa dhamana. Nitatoa uamuzi wangu kuhusu
maombi ya dhamana Jumatatu ijayo, hivyo naamuru washitakiwa warudishwe rumande,” alisema Msajili.

Washitakiwa hakuwatakiwa kujibu lolote. Mv Spice Islander ikiwa imesheheni mizigo na abiria kuliko uwezo wake, ilizama kilometa 10 kutoka pwani ya Nungwi wakati ikiwa njiani kwenda Pemba, usiku wa Septemba 9, mwaka huu.

Inaaminika kuwa wengi wa abiria 203 walikuwa watoto, waliokuwa wamelala chini wakati wa ajali. Hata hivyo, Tume maalumu itaundwa kuhusu ajali hiyo ambayo watu zaidi ya 600 waliokolewa.
 Uwezo wa meli hiyo ilikuwa ni kubeba watu 610. Katika hatua nyingine, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imetoa tamko la kusitishwa rasmi kwa kazi ya utafutaji wa miili ya watu walionasa kwenye vyumba vya meli ya mv Spice Islander kutokana na ugumu
wa utekelezaji wa kazi hiyo.

Kusitishwa kwa kazi hiyo kunatokana na kushindwa kwa wazamiaji wa kimataifa kutoka Afrika Kusini kuifikia meli hiyo kutokana na kina kirefu kilichopo eneo la ajali pamoja na hali mbaya ya hewa.

Akitangaza uamuzi huo wa SMZ, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd, alisema ingawa Serikali ilikuwa na nia ya kutaka kutolewa kwa kila miwili iliyonasa kwenye meli hiyo, lakini imeonekana kuwa kazi hiyo ni ngumu kutekelezeka.

Amewaomba Watanzania kukubali kuwa ndugu zao waliopoteza maisha na miili yao kushindikana kupatikana, ni mapenzi na uamuzi wa Mwenyezi Mungu aliyeamua kuwa bahari iwe sehemu ya makaburi ya ndugu zetu hao. Source Habari Leo

Friday, September 16, 2011

wabunge chadema wakamatwa kwa tuhuma za kumvamia mkuu wa wilaya

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Susan Kiwanga (Viti Maalum) na Sylivester Kasulumbai (Maswa Mashariki), wamehojiwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora wakituhumiwa kushiriki kumvamia na kumpiga Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Fatma Kimario.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Igunga, jana, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Mungulu, alisema wabunge hao walikamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa.
Akizungumzia kile kilichotokea, Mngulu alisema mkuu huyo wa wilaya alikwenda katika kijiji cha Isakamaliwa kufanya mkutano wa ndani na watendaji wa kijiji hali iliyowafanya wafuasi na viongozi wa CHADEMA kuchukizwa kwa madai kuwa wameingiliwa.
“Mkutano wa CHADEMA katika kijiji cha Isakamaliwa ulikuwa ufanyike kati ya saa nne na saa sita. Kikao cha mkuu wa wilaya kilifanyika kati ya saa 7:30 na saa 9:00 alasiri muda ambao CHADEMA hawakuwa na mkutano,” alisema.
Hata hivyo, kamanda huyo wa polisi alikiri kuwepo kwa malalamiko ya CHADEMA kuhusiana na kuingiliwa katika maeneo waliyotengewa kufanya kampeni na ukiukwaji wa maadili unaodaiwa kufanywa na mkuu huyo wa wilaya lakini akadai msemaji wa mambo hayo ni msimamizi wa maadili ambaye ni mkurugenzi wa uchaguzi.
Aidha alikiri kwamba askari wake walikuta hali ya amani na utulivu katika kijiji hicho, ndipo walipolazimika kuanza upelelezi kujua ukweli wa tukio hilo.
Aliongeza kuwa tuhuma zinazochunguzwa dhidi ya wabunge hao na wafuasi wengine watatu wa CHADEMA, ni kuvamia kikao cha mkuu wa wilaya.
Taarifa hizo zinadai kwamba katika tukio hilo mkuu wa wilaya alivuliwa hijabu, viatu, kukatiwa mkufu ambao thamani yake haijajulikana.
“Anadai kuwa simu yake ya mkononi aina ya Samsung yenye thamani ya sh 400,000 ilipotea na kumtukana matusi ya nguoni,” alisema na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa Ofisa Tawala wa Wilaya, Sumera Manoti.
Taarifa zimebainisha kuwa mkuu huyo wa wilaya amefungua jalada la shambulio la aibu namba IR/1115/2011, wakati CHADEMA wamefungua jalada namba IR/1115/2011 linalohusu kuingilia mkutano wa kampeni kwa mujibu wa ratiba ya msimamizi wa uchaguzi. Kwa sasa jeshi hilo linaendelea kukusanya ushahidi kuhusiana na kesi hizo.
Hata hivyo, Kamanda Mngulu alitoa wito kwa vyama, viongozi, wanachama, wapenzi na wafuasi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi hususan kipindi hiki cha uchaguzi.
Juzi mkuu wa wilaya hiyo akiwa katika kijiji cha Isakamaliwa, tarafa ya Igunga alivamiwa na viongozi, wafuasi na mashabiki wa CHADEMA muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani na watendaji wa vijiji.
Mbowe, Dk Slaa kuzunguka nchi nzima
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuanzia sasa yeye na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, watazunguka nchi nzima kuwahamasisha watu waikatae CCM na kuichagua CHADEMA.
Kauli hiyo aliitoa jana wilayani Sikongo, mkoani Tabora, alipofanya mikutano ya hadhara pamoja na kuzindua kampeni za udiwani wa kata ya Kisanga.
Dk. Slaa alisema binafsi ameamua kuacha kukaa ofisini baada ya kutembelea maeneo mengi ya nchi na kuona watu wanavyoishi kwa umaskini ilhali wamezungukwa na rasilimali lukuki.
“Moto tunaouwasha sasa CCM hawajawahi kuuona. Sitakaa ofisini mpaka kieleweke, taifa linahitaji ukombozi na sisi tuko tayari kuwakomboa wananchi,” alisema.
Dk. Slaa aliongeza kuwa Watanzania wako katika hali mbaya kwa sababu CCM imeshindwa kuzitumia rasilimali zilizopo kwa manufaa ya walio wengi.
Alisema umaskini unaowakabili wananchi hivi sasa si laana kutoka kwa Mungu bali ni maamuzi mabovu ya wananchi kuwachagua viongozi wenye kuweka mbele ulaji na maslahi binafsi.
“Tumebarikiwa rasilimali lukuki lakini wananchi tunapumulia mashine kwa umaskini, watu wetu wanaishi kwenye nyumba za tembe, hawajui bati wala umeme, hili halikubaliki hata kidogo,” alisema.
Dk. Slaa alisema kama Watanzania wanataka ukombozi ni lazima waache woga wa kuwachagua viongozi wa CCM ambao hawana uchungu wa matatizo ya wananchi.
Naye mgombea udiwani wa kata ya Kisanga, Mgombozi Ntewi (CHADEMA), alisema mabadiliko ya kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa hayawezi kufanyika kama wananchi wataendelea kuwa waoga.
Alisema iwapo atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo atahakikisha michango yote inayotolewa na wananchi inatumika kwa kazi zinazotakiwa.
“Maendeleo makubwa tutayapata iwapo mtanichagua kuwa diwani wenu; viongozi wetu wanatafuna fedha za miradi kwa manufaa yao, mimi nitawabana vilivyo,” alisema.

Mum acquitted of murdering four children

THE High Court in Kampala has acquitted a woman who pleaded guilty to strangling her four children to death, citing insanity.

Justice Andrew Bashaijja yesterday said at the time Margaret Kasande committed the crime, she was deranged. Reading the judgment yesterday, Bashaijja said prosecution had failed to prove that there was malice aforethought by the suspect.

Prosecution had alleged that Kasande on July 30, 2008 strangled her four children, who included a set of twins, at their home in Kamwokya, a Kampala suburb before trying to kill herself.

However, defence counsel Ambrose Tiishekwa, in his submission, insisted that Dr. Julius Muloni of Butabika Hospital in his report had stated that she had been mentally ill at the time.

Kasande pleaded guilty to murdering Marion Muhoozi, Batta Kabatsi, Medrine Nakato and Merisha Babirye and pleaded with court for a lenient punishment.

She said had lost her mind when she committed the murder and regretted the action because she loved her children. Kasande also asked for forgiveness from her husband and the country.

Bashaijja, in his judgment, ordered that the Ministry of Health take charge of Kasande at Butabika Hospital until she recovers from the mental problem she is suffering from.

Kasande’s estranged husband, Gerald Mukwandi, had asked court to make its verdict, but said he had forgiven her.

Mukwandi said their problems started when he stopped her from moving to Sudan where she had been promised a job.

Kasande, alias Nalongo, is said to have used a nylon curtain to strangle her daughters, aged between two and five, one by one, starting with the eldest.

She then placed the four bodies on a bed and covered them with a bed-sheet.

Kasande, in an attempt to commit suicide, put a rope around her neck and took poison, but was rescued by her husband when he returned from work in the evening.

Kampala bomber gets 25 years

                                       Nsubuga and Mugisha being led to prison
                                           Nsubuga and Mugisha being led to prison
By Andante Okanya and Edward Anyoli

THE two terrorists convicted for bombing Kampala in the July 11, 2010 twin bombings have been sentenced to 25 years and 5 years in jail respectively by the High Court in Kampala.

Edris Nsubuga was early Friday sentenced to 25 years each for the three counts of terrorism, while Muhamoud Mugisha was sentence to five years in prison for being a conspirator.

However, trial judge Alfonse Owiny-Dollo, ordered that Nsubuga will serve the 25 years for each count concurrently.

A total of 76 people perished in the two incidents that occurred at Kyaddondo Rugby Club and the Ethiopian Village Restaurant in Kampala. The third bomb that had been planted at the Makindye House on the same day was defused before it exploded.

However, at the first anniversary, the then deputy Inspector General of Police Julius Odwee, said over 100 people had subsequently perished.

Nsubuga and Mugisha who pleaded guilty to terrorism charges on Tuesday at the High Court, had been lined up by the Director of Public Prosecutions (DPP) to testify against the 12 other terror suspects.

The 12 other suspects are Hussein Hassan Agad, Idris Magondu, Isa Ahammed Luyima, Hassan Haruna Luyima, Abubakari Batematyo, Yahya Suleiman Mbuthia. Others are Habib Suleiman Njoroge, Omar Awadh Omar, Mohammad Hamid Sulaiman, Seleman Hijar Nyamandondo and Mohammad Ali Mohammad.

BREAKING NEWS PICHA NA MATUKIO YA KUUNGUA KWA SOKO LA MWANJELWA KIWANJA CHA SIDO

wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuungua kwa moto sopko la mwanjelwa
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka
Baadhi ya mabanda sokono hapo tayari yameteketea kabisa na moto
Kama kawaida kikosi cha zimamoto mbeya kimeendelea na maigizo yake ya kuja kwenye tukio na gari bovu hapa wanaonekana askari wa kikosi hicho wakibishana huku moto ukiendelea
Kufa kufaana kibaka tayari ameshaiba huyooo anatimka
Dada nae hayuko nyuma katika wizi keshachukua kapeti
Umati wa watu ukiwa unaangalia soko linavyoteketea
Mama huyu akilia kwa uchungu akiangalia duka lake likiteketea kwa moto

Picha na habari kwa hisani ya mbeya yetu blog

Chadema wamkamata Mkuu wa Wilaya Igunga

  

VURUGU zimezuka jana katika Kata ya Isakamaliwa, wilayani Igunga zikiwahusisha viongozi wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.Katika sakata hilo, wanachama wa Chadema walimkamata Mkuu huyo wa Wilaya kwa tuhuma za kuendesha mkutano wa ndani na watendaji wa serikali za vijiji, wakati akijua kuwa kulikuwa na mkutano wa kampeni za chama hicho karibu na eneo hilo.

Msafara wa Chadema ulifika katika eneo la kampeni saa 8.00 mchana na kabla mkutano haujaanza, Meneja Kampeni wa chama hicho, Sylivester Kasulumbai, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa wilaya ya igunga alikuwa akifanya kikao cha ndani katika eneo hilo kinyume na taratibu, hivyo wanakwenda kumshughulikia.

Kasulumbai ambaye ni Mbunge wa Maswa Mashariki akiwa na Mbunge wa Viti Maalum, Susan Kiwanga, baadhi ya wananchi na vijana wao, walifika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata kulikokuwa kunafanyika mkutano huo na kuanza kuhoji aliko Mkuu huyo wa Wilaya.

Mmoja wa wananchi alimnyooshea kidole mama ambaye alikuwa amekaa mbele na kusema; “..yule ndiye Mkuu wa Wilaya”.Kundi hilo la vijana na viongozi wa Chadema, waliingia katika ukumbi huo na kumtoa nje mama huyo huku wakimtaka aeleze kwa nini anafanya vikao vya ndani katika Kata hiyo wakati anajua kuwa chama hicho kilikuwa na mkutano katika eneo hilo.

Kitendo hicho kilizua purukushani na kutokuelewana kati ya waliokuwa kwenye mkutano wa ndani na viongozi wa Chadema, jambo lililovuta umati mkubwa wa watu.

Maelezo ya DC
Baadhi ya vijana wa Chadema walikuwa wamewashikilia watu waliokuwa wakishiriki mkutano huo huku mama huyo akitolewa nje na kuketishwa kwenye kiti alitakiwa atoe maelezo kuhusu mkutano wake.

Baada ya kukaa kwenye kiti huku akionekana kuchanganyikiwa, alisema yeye ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga, jina lake ni Fatma Kimario na kwamba, hakuwa na taarifa za mkutano wa kampeni za Chadema.

“Sina ratiba, iko katika ofisi za halmashauri, hivyo sikujua kama kuna mkutano hapa, hata hivyo watu walikuwepo niliwaruhusu waende mkutanoni na mimi nilikuwa naondoka sasa hivi,” alisema na kuongeza:

“Nilichokuwa nafanya ni mkutano wa viongozi wa serikali kwa ajili ya kuangalia hali ya mifugo inayoibwa sana, elimu kwa wote hasa watoto na ujenzi wa nyumba bora na masuala ya amani”.

Kimario aliwasihi wafuasi wa Chadema kusoma karatasi ya ajenda ili wafahamu kilichokuwa kikijadiliwa kwenye kikao hicho.

Karatasi aliyokuwa akiizungumzia Mkuu huyo wa Wilaya ilikuwa na ajenda tano za kikao hicho ambazo ni; Uhamishaji wa mifugo; Kuwa na choo chenye ubora na nyumba bora; Elimu; Mipaka ya shule na ajenda ya mwisho ilikuwa Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga.

Hata hivyo mbunge Kiwanga alimtaka mkuu huyo wa wilaya aeleze tangu lini kikao cha viongozi wa serikali kikahudhuriwa na wazee maarufu na mabalozi wa nyumba kumi, swali ambalo lilionekana kumchanganya mkuu huyo wa wilaya kwa kutoa majibu tata.

Mkutano wa Chadema
Wakati hayo yakiendelea, mkutano wa kampeni ulikuwa nao ukiendelea, hivyo viongozi hao wa Chadema walimtaka DC huyo afike kwenye mkutano huo ili aweze kuonana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Kimario alikubali, lakini akataka dereva wake atangulize gari na kwamba yeye angefuata. “Nitakwenda kwani napaswa kuwepo pale kama msimamizi wa usalama, sijahudhuria mkutano wowote hivyo nitakwenda,” alisema.

Akizungumzia tukio hilo kwenye mkutano wa kampeni, Dk Slaa alisema wakuu wa wilaya na mikoa kufanya mikutano wakati wa kampeni ni kinyume cha sheria, hivyo Kimario alienda kuanzisha vurugu.

“Hapaswi kufanya mkutano wowote hapa hasa akijua kuwa sisi tuna mkutano wa kampeni na yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Wilaya,” alisema Dk Slaa na kuongeza:

“DC anafanya nini huku wakati hiki ni kipindi cha uchaguzi au ndiyo wanapanga mikakati ya uchakachuaji halafu wanadai sisi ndiyo tunaofanya vurugu?”

Mkutano wa kwanza na wa pili wa Chadema, hakukuwa na ulinzi wa polisi kama ilivyokuwa kwenye mikutano mingine.

Askari wamwagwa
Wakati gari la waandishi wa habari likirejea mjini Igunga, lilipisha na magari mawili ya polisi yakiwa yamejaa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ambayo yalikuwa katika mwendo kasi yakielekea eneo la tukio.

Magari hayo yalifuatiwa kwa nyuma na gari aina ya Toyota Landcruiser ambalo lilikuwa na vioo vyeusi yote yakiwa yamewasha taa kuashiria hali ya hatari.

Hata hivyo polisi wilayani Igunga kupitia kwa Mkuu wake (OCD), Issa Maguha, waliliambia Mwananchi kuwa hawakuwa na taarifa ya tukio hilo na kwamba magari hayo yalikuwa katika doria za kawaida.

CCM yawaangukia wananchi

Katika hatua nyingine CCM kimewaangukia wananchi wa Igunga kikiwataka kuacha jazba na hasira kwani madhara ya kuchagua mbunge kwa chuki yataligharimu jimbo hilo kwa miaka minne ijayo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa NEC ya CCM Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Usongo kata ya Nyandekwa kinachoaminika kuwa ngome ya Chadema.

Habari zilizopatikana kijijini hapo kabla ya kuanza kwa mkutano huo zilidokeza kuwa Chadema walitangulia kufanya mkutano wa kampeni kijijini hapo na kumwaga ‘sumu’ ili wananchi waichukie na wasiichague CCM.

Akihutubia mkutano huo, Nchemba alirudia mara kadhaa kusema, “shusheni jazba” na “punguzeni hasira” ambayo ilitafsiriwa na wengi kuwa ni kujaribu kung’oa mizizi ya Chadema.

Katibu huyo alisema Chadema kimekuwa kikipandikiza chuki kwa wananchi kwamba Serikali ya CCM haijafanya lolote katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru. Alisisitiza kuwa huo ni uongo wa karne unaopaswa kupuuzwa.

“Kuwa na vuguvugu la kifikra inaruhusiwa na pia kuwa na mtizamo tofauti inaruhusiwa lakini si katika kipindi hiki ambacho wananchi wa Igunga wanahitaji mgombea wa CCM kuliko kipindi kingine chochote,” alisema.

Nchemba aliendelea kusema: ”kwenye uchaguzi mdogo nawaombeni mshushe jazba.…hata kama ulikuwa tayari na mlengo fulani, basi badilika kwa manufaa ya wana Igunga…, tusishabikie vyama bali tujadili hoja”.

Katibu huyo ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, aliwasihi wananchi wa kijiji hicho na Jimbo la Igunga kuacha kushabikia mambo ya maendeleo kama wanavyoshabikia timu za soka hata ambazo hawazijui.

Kwa upande wake, mgombea Ubunge wa CCM, Dk Dalaly Kafumu aliahidi kusimamia mradi wa kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria hadi Igunga kupitia majimbo ya Kahama na Nzega.

Dk Kafumu aliahidi kutumia utaalamu wake wa madini kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanatengewa maeneo yenye madini katika jimbo hilo na kutatua tatizo na kero ya muda mrefu ya daraja la Mbutu.

SOURCE MWANANCHI

BREAKING NEWS! Soko la sido Mbeya linateketea kwa moto hivi sasa

Soko la sido lililopo katika eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya linateketea kwa moto, taarifa za awali zimebainisha kuwa kikosi cha zimamoto kinafanya jitihada za kuuzima, hata hivyo chanzo cha moto huo bado hakijaelezwa, soko hilo ni chimbuko la lililokuwa soko la mwanjelwa lililoteketea kwa moto miaka mitano iliyopita. kwa taarifa zaidi ungana nasi baadaye

Thursday, September 15, 2011

Rais Kikwete ateua wakuu wa mikoa wapya 15



RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa nchini.
Katika mabadiliko hayo, amewateua Wakuu wa Mikoa wapya 15, kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa watano na wengine saba wamestaafu kwa mujibu wa taratibu. Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati Wakuu wa Mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine.
Aidha, Wakuu wa Mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Wakuu wa Wilaya 11 wamepandishwa Vyeo na kuwa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo: Bw. John Gabriel Tupa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara; Bw. Saidi Thabit Mwambungu (Ruvuma); Bi. Chiku S. Gallawa (Tanga); Bw. Leonidas T. Gama (Kilimanjaro); Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma); Bw. Elaston Mbwillo (Manyara); Kanali Fabian Massawe (Kagera); na Bibi. Fatma Abubakar Mwassa (Tabora). Wakuu wa Wilaya wengine walioteuliwa ni Bw. Ali Nassoro Rufunga, (Lindi); Eng. Ernest Welle Ndikillo, (Mwanza); na Bw. Magesa Stanslaus Mulongo Mkuu wa Mkoa (Arusha).
Walioteuliwa nje ya nafasi hizo ni Eng. Stella Manyanya (Rukwa); Bibi Mwantumu Mahiza, (Pwani); Bw. Joel Nkaya Bendera (Morogoro) na Bw. Ludovick Mwananzila (Shinyanga).
Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Bw. Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza; Bw. Said Mecki Sadiki anayekwenda Dar es Salaam akitokea Lindi; Bibi Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma; Lt. Kanali Issa Machibya anayekwenda Kigoma akitokea Morogoro; na Kanali Joseph Simbakalia anayekwenda Mtwara akitokea Kigoma. Dk. Parseko Ole Kone ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Waliostaafu ni Bw. Mohammed Babu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera; Bw. Isidore Shirima aliyekuwa Arusha; Kanali (mst.) Anatory Tarimo aliyekuwa Mtwara; Bw. John Mwakipesile, aliyekuwa Mbeya. Wengine ni Kanali Enos Mfuru aliyekuwa Mara; Brig. Jen. Dk. Johanes Balele aliyekuwa Shinyanga; na Meja Jen. Mst. Said S. Kalembo aliyekuwa Tanga.
Wakuu wa Mikoa wanne waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma; Bw. Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Bw. Daniel Ole Njoolay aliyekuwa Rukwa.
Wakuu wote wa Mikoa waliopo sasa wameagizwa kuandaa Hati za Makabidhiano (Handing Over Notes) katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa Wakuu wapya wa Mikoa. Aidha Wakuu wa Wilaya ambao wamepandishwa vyeo kuwa Wakuu wa Mikoa nao wanapaswa kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.
Wakuu wa Mikoa ile minne mipya na Wakuu wa Wilaya watakaoteuliwa hapo baadaye nao watatakiwa kuandaa Hati za Makabidhiano ndani ya siku 14 tangu kuapishwa.
Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao.
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa na Wakuu wa Mikoa minne mipya wakaoteuliwa pamoja na Wakuu wote wa Wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.
Wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa siku ya Ijumaa, Septemba 16, 2011 saa 4.00 asubuhi kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kusaini Mkataba


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA) Suleiman .S,Suleiman (kushoto miwani) pamona na Mhandisi Mwandamizi wa Kampuni ya SINOHYDRO CORPORATION LTD Tawi la Afika Mashariki Qin Chao wakitiliana saini mikataba ya ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Kigoma, katika sherehe iliyofanyika jijini Dar es salaam Sept,15,2011 ikiwa katika muendelezo wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara katika sekta ya Uchukuzi, Sherehe hiyo pia imehudhuriwa na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi,Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

JK Ampokea Rais Wa Visiwa Vya Comoro


1. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Umoja wa visiwa vya Comoro Dr.Ikililou Dhoinine katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo mchana.
 
2. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Umoja wa visiwa vya Comoro Dkt.Ikililou Dhoinine muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana(Picha : Freddy Maro).

Wednesday, September 14, 2011

Yemen takes back strategic southern capital from Al Qaida


 
 The Yemen Army announced the capture of the southern provincial capital of Zinjibar on Sept. 10. The Army said Al Qaida, in control of the coastal city since May, fled Zinjibar amid heavy artillery and air strikes.
'The kingdomof Saudi Arabia and the United Statesgovernment provided logistical support during the ongoing operations,' a Yemeni government statement said.
Officials said Riyad and Washington joined in air strikes and flew supplies to the embattled Yemen Army around Zinjibar. They said the foreign aid allowed the Army's 25th Brigade to break out of an Al Qaida siege that lasted nearly five months.
The Defense Ministry said at least 280 people were killed in fighting between the brigade and AQAP. The ministry said most of the casualties, more than three times the figure previously released by Sanaa, consisted of Yemeni soldiers.
'The southern military region lost more than 230 martyrs in the fighting,' Defense Minister Mohammed Nasser Ahmed said.
Zinjibar, the capital of Abyan, has long been regarded as a strategic location. Yemenemploys the coastal city for the transport of three million barrels of crude oil per day.
Still, Al Qaida in the Arabian Peninsula remains deployed in Abyan, including partsof Zinjibar.
Officials said AQAP was regrouping in Jaar, located near Zinjibar.
'We are pursuing limited pockets of militants,' Yemen Army Gen. Mohammed Al Somali said. 'But the real battle will be to cleanse the town of Jaar.'
Officials said President Ali Abdullah Saleh congratulated the Army from Saudi Arabia. Saleh has been confined to Saudi Arabia since June when he was flown for medical treatment in wake of a bombing of his compound.
Source: World Tribune

Miss universe apatikana ni Leila Lopes Kutoka Angola







Miss Universe 2011 ilifanyika juzi tarehe 12 september huko San Paolo, Brazil.Watanzania tuliwakilishwa na Nelly Kamwelu

Tuesday, September 13, 2011

Top 10 Tourist destinations

1. Ngorongoro Crater
2. Serengeti National Park
3. Zanzibar and Pemba
4. Tarangire National Park
5. Lake Manyara National Park
6. Mt. Kilimanjaro
7. Selous Game Reserve
8. Ruaha National Park
9. Mafia Island
10. Mt. Meru

http://www.tanzaniatouristboard.com

The highest peak and most famous mountain in Africa (Mount Kilimanjro)


The highest peak and most famous mountain in Africa, scaling the peak of Mount Kilimanjaro is a heavy challenge, more from the rigours of altitude than the actual difficulty of the hike itself. The climb, which takes on average five days ( you're more likely to reach the top if you pace yourself), takes hikers through thick forests and alpine grasslands, desolate rockface and brilliant white glaciers.
Views of Kenya and the Masaai Steppe, the Crater Highlands, and the Eastern Arc Mountain Range expand from the summit, and unlike other comparable peaks, you don't need ropes or climbing equipment to make it to the top. As long as you pace yourself and take it easy at high altitudes, you have every reason to think you can. Visit http://www.tanzaniatouristboard.com/

Republicans tackle Obama’s jobs plan

IOL pic sep14 barack obama jobs plan
Associated Press
President Barack Obama's jobs plan is being criticised by Republicans in Congress, but he is determined to sell the $447-billion proposal while on the road in the coming weeks.
Washington - Republicans in Congress on Tuesday intensified their criticism of President Barack Obama's jobs plan as he hit the road to sell the $447-billion proposal as the best hope to boost the struggling US economy
.
New government figures underscored the challenges Obama and US lawmakers face in attempting to trigger growth in a US economy still recovering from the worst recession since the Great Depression.
The Census Bureau said the number of Americans living below the poverty line rose to a record 46-million last year, with the national poverty rate climbing for a third consecutive year to 15.1 percent in 2010.
Obama's plan to bring down a stubbornly high 9.1 percent jobless rate with a package of tax cuts and spending paid for entirely by tax hikes on the wealthy and corporations came under renewed fire from Republicans in Congress.
“What the president's proposed so far is not serious. And it's not a jobs plan,” Senate Republican leader Mitch McConnell said in a speech on the Senate floor. Obama sent the job legislation to Congress on Monday.
Speaker of the House of Representatives John Boehner, the top Republican in Congress, was equally sceptical, saying, “I just don't think that is really going to help our economy the way it should.”
Obama hit the road to Columbus, Ohio, in Boehner's political backyard, to sell the plan. It was an opportunity to talk up his proposal in an important battleground state as he looks ahead to what is shaping up to be a difficult battle for re-election in November 2012.
hostgator coupon code