Saturday, September 10, 2011

Picha ya MV. Spice Islander Ilivyozama

 

Nadhani vyombo vingi tayari vimeshaanza kutowa taarifa za ajali ya meli ya Mv. Spice Islander katika safari yake kuelekea kisiwani Pemba.
Inasemekana abiria waliomo ni kadiri ya 600 lakini wengi wana wasiwasi kwamba wanaweza wakazidi ya hapo ukichukulia idadi hiyo ni idadi ya kawaida ya abiria kwa boti ndogondogo za mwendo wa kasi kama Kilimanjaro za Bakhressa.
Mpaka saa nne asubuhi, waliokolewa wanakadiriwa kuwa ni 490 na waliokufa ni takriban 40 lakini mpaka hivi sasa kwa mujibu wa nambari zionyeshwavo kupitia Zanzibar Broadcasting Cooperation (ZBC) ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la TVZ, idadi inakadiriwa kufikia 120 na bado inaendelea. Tunamuomba Mwenye Enzi Mungu awalaze mahala pema peponi, Aaamin.
Picha na taarifa vimetumwa na mwenzetu Abdulahman Abdulahman kupitia mtandao wa Wanabidii.

No comments:

Post a Comment

hostgator coupon code