Tuesday, August 30, 2011

DK KAFUMU NDIYE MGOMBEA WA CCM KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA IGUNGA


kamati kuu ya CCM ilikaa jana siku ya jumatatu na kumchagua Dk Dalalay Peter Kafumu kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo wa Igunga,Tabora. Dk Kafumu ni kamishina wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini ambapo katika uchaguzi huo alipita kwa 68% kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye, uchaguzi huo unafuata baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kujiuzulu.

WAZIRI MAMBO YA NJE AKUTANA NA BALOZI WA LIBYA TANZANIA



Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana amemwita ofisini kwake Balozi wa Libya nchini Prof. Ahmed Al Ash'hab. Kisa? Ubalozi huo umebadilisha bendera ya Libya, kuondoa iliyokuwa ikitumika enzi za Gaddafi na kuweka inayotumiwa sasa nchini Libya. Ubalozi huo unaambiwa umefanya hivyo bila kufuata utaratibu. Je, hii imekaaje? Picha na Tagie Mwakawago wa Mambo ya Nje.

WAZIRI MAMBO YA NJE AKUTANA NA BALOZI WA LIBYA TANZANIA



Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana amemwita ofisini kwake Balozi wa Libya nchini Prof. Ahmed Al Ash'hab. Kisa? Ubalozi huo umebadilisha bendera ya Libya, kuondoa iliyokuwa ikitumika enzi za Gaddafi na kuweka inayotumiwa sasa nchini Libya. Ubalozi huo unaambiwa umefanya hivyo bila kufuata utaratibu. Je, hii imekaaje? Picha na Tagie Mwakawago wa Mambo ya Nje.

ANSWAAR SUNNA WASWALI SWALA YA EID LEO KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI


sheikh juma poli amir akiongoza swala ya Eid leo katika viwanja vya jangwani leo jijini Dar-es-salaam


waumini wa madhehebu ya Answaar sunna wakisikiliza mawaidha leo katika viwanja vya jangwani wakati wa ibada ya Eid

kwa hisani Michuzi blog

TTCL YATOA MISAADA KWA SHULE YA MSINGI UHURU MCHANGANYIKO NA KITUO CHA SOS KWA AJILI YA SIKUKUU YA EID EL FITR

 
 
Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Mrisho Shaban (kushoto) akimkabidhi msaada wa vyakula Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Juma Lukinga kwa ajili ya sikukuu ys Eid El Fitr wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika shule hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo
 
 
Na Francis Dande
KAMPUNI ya simu Tanzania (TTCL) leo imetoa msaada wa vyakula kwa watoto walemavu wa shule ya Uhuru mchanganyiko pamoja na wasiojiweza katika kituo cha SOS kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi misaada hiyo vyenye thamani ya shilingi mil 3.5. ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Mrisho Shaaban alissema msaada huo unalenga kusherehekea sikukuu ya Idd Elfitr pamoja na watoto ambao kwa namna moja ama nyingine ni kundi linalohitaji kusaidiwa na jamii inayoizunguka.
“Sisi TTCL kama kampuni ya umma na ya kizalendo tunajali sana jamii inayotuzunguka pamoja na matatizo yake ndio maana leo tunatoa msaada wa vyakula kwa makundi haya ya watoto wahitaji kwa kuwa in jukumu letu kama kammpuni ya kitanzania kusaidia,”alisema Shaaban.
Alisema mbali na kutoa misaada kwa Uhuru na SOS lakini pia tayari wametoa misaada kama hiyo kwa vikundi vya wazee , yatima na walemavu wa viungo vya mwili mjini Moshi ambapo vikundi vitatu kila kimoja kilipatiwa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.
“Tunaahidi kuendelea kuhudumia jamii yetu pale kampuni inapofanya vizuri na mapato kuongezeka kwani ndio njia mojawapo ya kurudisha baadhi ya mapato tuliyokusanya kwa wateja wetu ,”alisema Shaaban.
Aidha aliwaomba watanzania kuendeleza ushirikiano na kampuni hiyo katika kupinga hujuma zozote dhidi ya mtandao na kampuni ya TTCL kwa ujumla.
Naye mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Juma Lukinga alisema sio mara ya kwanza kupokea misaada mbalimbali kutoka kwa TTCL na kwamba anamshukuru mungu kwa kuwa misaada hiyo inawasaidia sana kutokana na hali ngumu ya maisha iliyopo.
Alisema misaada hiyo itawasiaida kula na watoto katika sikukuu ya Idd na kwamba watajiona wanafuraha sawa na watoto wengine .

SERIKALI YA JAPANI YAIPA TANZANIA BILIONI 40 KWA AJILI YA UJENZI WA DARAJA LA LUSUMO NA BARABARA JIJINI DAR-ES-SALAAM

 

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (leo) jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini msaada wa shilingi bilioni 40 kwa ajili ya miradi miwili ya maendeleo. Mradi wa kwanza ni ujenzi wa daraja la Rusumo lilopo mpakani wa Tanzania na Rwanda na uimarishaji wa barabara jijini Dar es salaam. kulia ni Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam

Na Hadija Chumu na Moshi Stewart-Maelezo,Dar es Salaam
Serikali imesaini msaada wa shilingi bilioni 40 na serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miradi miwili ya maendeleo hapa nchini.

Akiongea na wanahabari leo Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo amesema miradi hiyo ni ya ujenzi la wa daraja la Rusumo litakalounganisha nchi ya Tanzania na Rwanda na upanuzi wa barabara ya Kilwa ambapo itasaidia shughuli za maendeleo baina ya nchi hizo.
Waziri Mkulo alisema
Alisema upanuzi wa barabara ya kilwa utapunguza kwa kiasi kikubwa foleni na adha nyingine za kimiundombinu ndaji ya jiji la Dar es salaam,
Nae Balozi wa Japani nchini Bw Hiroshi Nakagawa amesema msaada huo ni matokeo ya ushirikiano uliopo kati ya Japani na Tanzania ambapo utasaidia kuimarisha uchukuzi na usafirishaji nchini,
Balozi Nakagawa alisema kiasi cha bilioni 1.86 za kijapani zitasaidia upanuzi wa daraja la Rusumo, wakati Yen Milioni 37 zimetolewa kukamilisha upanuzi wa barabara ya kilwa
Nae mwakilishi wa shirika la JICA nchini Bw Yukihide Katsuta amesema fedha zilizotolewa na shirika hilo ni milioni 769 za kitanzania ambazo zitasaidia kupata mwongozo sahihi wa kitaalam utakaopelekea ubora katika ujenzi na upanuzi wa barabara ya kilwa unaotegemea kukamilika hivi karibuni
Aidha mwakilishi wa TANROADS Mhandisi Mfugale amesema watahakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati na ubora unaohitajika ili kuhakikisha na kusimamia upanuzi wa daraja hilo pamoja na ule wa upanuzi wa barabara ya kilwa unatimizwa kulingana na fedha zinazotolewa.

Sunday, August 28, 2011

Rooney scores hat-trick as United hit eight past Arsenal

                                

 Wayne Rooney scored a hat-trick as champions Manchester United retained their 100% English Premier League record this season with a remarkable 8-2 thumping of injury-hit Arsenal at Old Trafford.

United dominated the Gunners who suffered their worst ever Premier League defeat.


With Manchester City winning 5-1 at Tottenham also on Sunday, it proved a superb day for the two Manchester clubs, who are level at the top with a maximum nine points from their three games.

Bolt sensationally disqualified as Blake wins 100m

Defending champion Usain Bolt was sensationally disqualified for a false start in the men's 100m final at the world athletics championships in Daegu, South Korea, allowing fellow-Jamaican Yohan Blake to collect an unexpected gold medal.
Bolt has dominated men's sprinting since winning 100m and 200m gold at the Beijing Olympics in 2008, achieving the same feat at the world championships in Berlin the following year -- smashing the world record in the process.
And although he had not entered this year's worlds in top form, the absence through injury of rivals Asafa Powell and Tyson Gay meant he was hot favorite to retain the first part of the sprint double.

However, the 25-year-old fell foul of the current false start rules, which states that once one false start has occured, the next athlete to jump the gun is immediately disqualified
.
"I can't find words to explain it. Usain Bolt has been there for me. I feel like I want to cry," Blake told reporters. "I felt I would win the race for Bolt."

Wikileaks leaks Dar`s cables

After being silent for months, Wikileaks, a global whistleblower website is back at it this week, releasing over 100 US secret State Department cables about Tanzania filed between 2005 and 2010.
Some 20,000 documents were made available from the cable trove between Wednesday and Friday morning, and a Friday tweet from WikiLeaks promises 45,000 more will come soon. These numbers are still developing.
In perhaps the biggest batch of cables about Washington’s views about the Dar es Salaam regime under President Kikwete, the cables touche various issues from politics to economics, terrorism, human rights and the media.
However majority of these cables are unclassified and only two cables, the one about the smuggling of Uranium from Democratic Republic of Congo to Iran via Dar es Salaam port, and the corruption dossier, are classified.
In one of the cables filed to Washington, the US government described President Jakaya Kikwete as pro-Westerner, charismatic, and a friend of the world’s most powerful nation.
The cable was filed just a few days after Kikwete was elected to be the fourth President of the United Republic of Tanzania in November, 2005.
But, this view seemed to conflict with what the US embassy reported back to their country, four years since President Kikwete came into power.
In its cable filed in 2009, US claims that President Kikwete’s regime was failing to deliver contrary to the expectations, citing massive corruption within the government as well as growing frustration among Tanzanians. The cables also aired the view about the closure of a Ponzi scheme known as Deci, which during its closure was worth $10 million, with an estimated 700,000 members countrywide.
“Although all indications point to Deci Tanzania being a Ponzi scheme, among investors the most controversial issues surrounding it was the government’s decision to close it down…some theories propounded by unhappy investors include that Tanzanian leadership was was angry that traditional banks and investment opportunities would lose out to Deci,” reads part of the cables.
The cable further adds that the government was angry because Deci was a Christian and not a Muslim organisation.
Citing drug trafficking, the cables brand Tanzania as the ‘main conduit’ for drugs to Southern African countries due to its porous borders, seaports and airports.
The cables also blame lack of control at Zanzibar’s ports and airports, adding that the loopholes pave the way for the Indian Ocean archipelago to be the heaven of drug traffickers.
In general most of the leaked cables have very few ‘toxic materials’ that may hamper the growing relationship between Washington and Dar es Salaam.
SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY
 

Saturday, August 27, 2011

MAMA SALIMA KIKWETE AENDESHA HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWAAJILI YA TAMASHA LA MOWE



Mwenyekiti wa Taasisi wa WAMA pia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Wajasiriamali Aug 26,2011 jinini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) 2011 litalofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mwaka huu Taasisi ya WAMA ndio mratibu wa Tamasha hilo.Jumla ya zaidi milioni 55 zimechangwa katika hafla hiyo na kauli mbiu ya mwka huu ya MOWE ( MIAKA 50 WANAWAKE WAJASIRIAMALI TUNAWEZA-TUTUMIE FURSA),(kulia ni Mwenyekiti wa MOWE Tanzania Elihaika Mrema,na (kushoto) ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Consolata I.

Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Alexio Musindo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) yaani Month of Women Enterprenuers,

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea vitabu kutoka kwa muwakililishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania Gloria Kavishe(kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa uchangiaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) August 26,2011, Vitabu hivyo vimekabidhiwa kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule ya mfano ya watoto yatima WAMANAKAYAMA iliopo Rufiji mkoa wa Pwani,

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mwakilishi wa Bank ya CRDB (kulia)kwaajili ya kuchangia tamasha la wajasiriamali wanawake (MOWE) 2011 , (aug 26,2011)) jijini Dar es Salaam, Zaidi ya shiligi 55 milioni zimechangwa.(55,368,500/)

Baadhi ya Wanawake wajasiriamali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Slama Kikwete (Aug 26,2011) katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) jijini Dar es Salaam

Picha ya pamoja ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya MOWE na vbaadhi ya viongozi wa meza kuu akiwepo Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO

VODACOM MISS TANZANIA NDANI YA JANGWANI SEE BREEZE TAYARI KWA BONANZA


Hapa wakipima moja ya mavazi ambayo watayatumia katika shindano la Vodacom Miss Tanzania litakalofanyika Sptemba 10/2011.


Warembo wanaoishiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakiingia katika ufukwe wa Jangwani See Breez ambako leo kunafanyika tamasha la michezo la Vodacom Miss Tanzania Sports Day, ambapo watashiriki kucheza michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kuvuta Kamba, Kukimbia na Magunia, Kuchezo Soka, Kucheza mpira wa Pete na Mpira wa wavu. Shindano la Vodacom Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika Septemba 10/2011 kwenye ukumbi wa Malimani City Jijini Dare es salaam Tanzania.



Washiriki Wakiendelea Kushuka Kwenye gari lao tayari kwa ushiriki katika bonanza


Picha Na Habari Kwa Hisani Ya John Bukuku - Full Shangwe Blogu

Friday, August 26, 2011

VODACOM TANZANIA NA MAONESHO YA SEKTA YA MAWASILIANO


Rais Dk.Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Meneja mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw Salum Mwalim jinsi ambavyo Vodacom inavyochangia maedeleo ya vijijini kupitia teknolojia ya simu ya mkononi ikiwemo huduma ya m-pesa na MWEI huku akipitia jarida la Vodacom alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya wadau wa mawasiliano ya simu yanayofanyika sanjari na mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa sekta ya mawasiliano barani Afrika - CTO. jijini Dar es salaam ambao Vodacom ni mdhamini.


Rais Dk. Jakaya Kikwete akioneshwa na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim fulana ya Vodacom yenye logo na rangi mpya za kampuni hiyo tangu ilipobadilika kutoka buluu kuwa nyekundu Aprili Mwaka huu wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maoensho ya sekta ya mawasiliano yanayofanyika sanjari na mkutano wa mwaka wa wadau wa mawasiliano ya simu barani Afrika jijini Dar es salaam jana ambao Vodacom ni mdhamini.
Mkuu wa Huduma za kifedha wa kampuni ya Vodacom Jacques Voogtz akiwasilisha mada juu ya njia za kusaidia maendeleo vijijini kupitia teknolojia za mawasiliano ya simu katika mkutano wa mwaka wa taasisi ya mawasiliano ya Jumuiya ya Madola - CTO unaofanyika jijini Dar es salaam. huduma ya m-pesa imekuwa mfano mzuri wa ukombozi wa kimawasiliano katika nyanja ya kifedha kwa wananchi vijijini hapa nchini.

JUMLA YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 777 ZIMETENGWA KUKAMILISHA MPANGO WA UNDAP 2011-2015.



Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akifungua rasmi semina ya waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania nchini, juu ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) Semina imefanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akiwakaribisha wadau na waandishi wa habari katika semina hiyo.
Mtaalamu wa Masuala ya Kulinda Haki za Watoto wa UNICEF Mona Aika akitoa maelekezo kwa Mwandishi wa habari wakati wa semina ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP).
Mmoja wa watumishi wa IAGG Bi. Salome Anyeti akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya masuala ya Haki na Jinsia katika mwendelezo wa semina iliyoandaliwa na UN Tanzania kwa lengo la kuhamasisha waaandishi wa habari kuandika na kuelimisha jamii juu ya mpango wa MKUKUTA na MKUZA kwa kipindi cha miaka 4 ijayo. Kushoto ni Bw. Robert Basil Mwenyekiti wa IAGG upande wa Jinsia na Maambukizo ya Ukimwi kutoka kitengo cha Chakula na Kilimo UN.
Mratibu wa Ukuaji Uchumi kutoka FAO Dkt. Vedasto Rutachokozibwa akibadilishana mawazo na waandishi wa habari katika Semina ya UNDAP iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa UNHCR Juliana Bwire akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango mzima wa UNDAP kwa upande wa sekta ya wakimbizi ambayo Mwakilishi Mkazi wa UN nchini Alberic Kacou amesisitiza ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Afisa Program wa WFP Said Johari na Afisa Uhusiano wa michango wa WFP Fizza Moloo wakizungumza na mwandishi wa habari alitembelea kitengo hicho wakati wa semina ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assitance Plan 2011-2015 (UNDAP).

BENKI YA NBC YACHANGIA KWA WANAMICHEZO WA TANZANIA WATAKAOSHIRIKI ALL AFRICA GAME


Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC Tanzania, Robi Matiki-Simba (kulia) akikabidhi tiketi saba za ndege za kwenda na kujrudi Msumbiji kwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Kanali Iddi Kipingu kwa ajili ya timu ya Tanzania ya wanamichezo wenye ulemavu inayotarajiwa kushiriki michuano ya Afrika ya All Africa Games nchini Msumbiji kuanzia Septemba 3 mwaka huu. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania, Iddi Kibwana.
Baadhi ya timu ya Tanzania ya Paralimpiki wakipozi kwa picha na Kanali Kipingu, Meneja Uhusiano wa NBC, Bi. Robi na Katibu Mkuu wa TPC, Iddi Kibwana katika hafla hiyo.
Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC Tanzania, Robi Matiki-Simba (kulia) akishikana mikono na mwanamichezo mwenye ulemavu, Bernadeta Kinyelo baada ya kukabidhi iketi saba za ndege za kwenda na kurudi Msumbiji kwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezom la Taifa (BMT) Kanali Iddi Kipingu (wane kulia waliosimama) kwa ajili ya timu ya Tanzania ya wanamichezo wenye ulemavu inayotarajiwa kushiriki michuano ya Afrika ya All Africa Games nchini Msumbiji kuanzia Septemba 3 mwaka huu. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

WAZIRI MKUU JAPANI ATANGAZA KUJIUZULU




Waziri mkuu wa japani Naoto Kan ametangaza kujihuzulu rasmi baada ya kiwango cha kukubaliwa kwake kushuka kutokana na majanaga yaliyoikumba japani ya tetemeko la ardhi na tsnami, ametangaza kujiuzulu ijumaa. Kan alitangaza kujiuzulu kwake katika mkutano na wanachama wa chama tawala cha Democratic cha nchini japani. Kan amekuw a akishinikizwa ajiuzulu toka march 11,kufuatia matetemeko ya ardhi na tsunami ilyoikumba nchi hiyo pamoja na kuvuja kwa mionzi ya nuclear nchini humo

Thursday, August 25, 2011

WAKE WA MABALOZI WAIPA GARI HOSPITALI YA AMANA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wake na Waume wa mabalozi wa nchi za Afrika waliopo nchini, Aletha Isaack (kushoto) akikabidhi funguo za gari la wagonjwa kwa Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya na


Serikali imesifu jitihada zinazochukuliwa na wake za mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini katika kuhakikisha vifo vya akinamama na watoto vinapungua.
Akizungumza wakati akipokea msaada wa gari la wagonjwa kutoka umoja wa wanawake hao jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Magreth Mbando, alisema nguvu zao zitaongeza kasi ya utoaji tiba huduma ya uzazi salama.
Gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 11 limetolewa kwa ajili ya kutoa huduma katika Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala.
Dk. Mbando alisema hospitali hiyo inawahudumia watu 29,000 katika huduma ya uzazi kwa mwaka ambayo ni wastani watu 60 hadi 100 kwa siku. Wagonjwa wanaopatiwa rufaa ya kwenda muhimbili ni kati ya watu watatu hadi sita kwa siku.

kwa hisani ya Nipashe

SIMBA WALIVYOTINGA BUNGENI DODOMA JANA NA NGAO YAO YA JAMII



Wachezaji wa Simba SC Bungeni Dodoma leo na Ngao yao ya Jamii waliyoishinda kwa kuifunga Yanga bao 2-0 katika mchezo wa kufungua pazia wa ligi kuu ya Vodacom
Ngao ya Jamii iking'ara mjengoni
Ankal ndani....dah!
Wachezaji na maafisa
Felix Sunzu (kulia) na afisa wa Simba
Kocha wa makipa Iddi Pazi 'Faza' akiwa mjengoni na vijana
Nahodha Juma Kaseja akiwa kashikilia Ngao ya Jamii mjengoni
Simba wakitoka mjengoni wakiwa wamezongwa na mashabiki wao
Picha ya Pamoja na waheshimiwa
Furaha tupu Bungeni Dodoma leo
Waziri wa Ardhia Profesa Anna Tibaijuka na Mbunge wa Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Simba Mh Ismail Aden Rage wakipozi na 'watoto'
Taswira zote kwa Hisani ya Issa Michuzi Blog

WASHIRIKI WA SHINDANO LA VODACOM MISS TANZANIA WAPIGWA MSASA JUU ZA HUDUMA ZA VODACOM M-PESA

Meneja Huduma wa Bidhaa za Vodacom, Elihuruma Ngowi akifafanua jambo juu ya huduma ya M Pesa kwa washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika kambi yao iliyopo jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Utawala wa Huduma ya M Pesa kutoka Vodacom, Emmanuel Pallangyo akigawa viperushi vilivyo na maelezo ya namna huduma ya M Pesa kwa washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika kambi yao iliyopo jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam jana
Baadhi ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakijisajili katika huduma ya M Pesa baada ya kupata semina juu ya faida na umuhimu wa kuwa umejisajili katika huduma hiyo jana wakiwa Kambini katika Jumba la Vodacom
Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipiga picha na mabaunsa waliovalia vazi la M Pesa “Super Man” baada ya warembo hao na wenzao kupata semina juu ya faida na umuhimu wa kuwa umejisajili katika huduma ya M Pesa jana wakiwa Kambini katika Jumba la Vodacom.
hostgator coupon code