Saturday, October 8, 2011

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Petrobras, Bw. Fernando Jose Cunha

5527 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Petrobras, Bw. Fernando Jose Cunha kwenye Ofisini kuu ya kampuni hiyo, Rio de Janeiro akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil Oktoba 7,2011. Kampuni hiyo imeanza kazi ya kutafuta mafuta kwenye pwani ya Mtwara nchini.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Petrobras, Bw. Fernando Jose Cunha (kushoto kwake) kwenye Ofisini kuu ya kampuni hiyo, Rio de Janeiro akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil Oktoba 7,2011. Kampuni hiyo imekwishaanza kutafuta mafuta kwenye pwani ya Mtwara. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi, Maendeleo ya Makazi, Maji na Madini wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary Nagu na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
5513 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Uongozi wa juu wa Kampuni ya Mafuta ya Petrobras kwenye Ofisini kuu ya kampuni hiyo, Rio de Janeiro akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil Oktoba 7,2011 Kampuni hiyo imekwishaanza kutafuta mafuta kwenye pwani ya Mtwara.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ahudhuria Mkutano wa Afrika na Asia katika harakati za kumsomesha mwanamke

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akihutubia Mkutano wa Afrika-Asia 2011 leo ambapo amesisitiza elimu yenye maadili ndiyo njia pekee ya kumkomboa mwanamke pamoja na jamii kwa ujumla. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Wanawake cha Sookmyung nchini Korea Kusini ambacho kimetiza miaka mia moja na tano tangu kianzishwe 1906.
Salma Dinya ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ambaye alialikwa kwenye mkutano huo kuiwakilisha Tanzania kama kiongozi kijana. Hapa anatoa mada kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Asia na Afrika kuhusu Tanzania.
Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Korea katika Vyuo Vikuu mbalimbali walifika kumsikiliza spika wao

Thursday, October 6, 2011

Rais Kikwete Akagua Uzalishaji Umeme Bwawa La Kidatu

 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mitambo ya kuzalisha umeme katika bwawa la Kidatu,mkoani Morogoro jana .Kushoto ni meneja wa TANESCO wa mkoa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera
(picha na Freddy Maro).

WAZIRI MKUU ZIARANI NCHINI BRAZIL

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Mhe. Eddison Lobao (kulia) October 5, 2011 kwenye Ofisi za wizara hiyo zilizoko Brasilia. Yuko katika ziara ya kikazi nchini humo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu picha ya wafugaji wa kabila la Wamasai aliyomzawadia Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Mhe. Eddison Lobao (kushoto) October 5, 2011 baada ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za wizara hiyo zilizoko Brasilia. Yuko katika ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Mary Nagu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Mhe. Eddison Lobao (kulia) October 5, 2011 kwenye Ofisi za wizara hiyo zilizoko Brasilia. Yuko katika ziara ya kikazi nchini humo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Waziri wa Kilimo, Mifugona Ugavi Mhe. Jorge Alberto Portanova wakati alipowasili kwenye ofisi za Wizara hiyo zilizoko Brasilia kwa mazungumzo ya kiserikali akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, October 5, 2011.

Monday, October 3, 2011

RAISI MUSEVENI ATUA DAR ES SALAAM NA KUPOKELEWA NA RAISI KIKWETE


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakikagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakikagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo ikulu jijini Dare s Salaam leo mchana.Rais Museveni yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akimkaribisha Rais wa Uganda Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni (kulia) leo jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kikazi nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiongozana na mgeni wake Rais wa Uganda Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni (kulia) leo jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kikazi nchini Tanzania kupita katikati ya gwaride maalum liloandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Said Mwema(kushoto) akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni leo jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kikazi nchini Tanzania.((Picha na Tiganya Vincent/Freddy Maro)

Sunday, October 2, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU YA WIZARA YA AFYA YAFUNGWA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin.
Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin akizungumza wakati wa kufungwa kwa maadhimisho hayo ambapo ameipongeza Tanzania kwa Mafanikio iliyofikia katika utoaji huduma za Afya katika Kipindi cha Miaka 50 iliyopita haswa katika kupunguza vifo vya watoto wadogo ambapo Tanzania kwa sasa imefanikiwa kupunguza vifo 110.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Idara mbalimbali za Wizara ya Afya wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara hiyo. Mhe. Lucy Nkya
Mgeni rasmi akiongea na baadhi ya Wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma za Upimaji na Matibabu ya Masikio, Koo na Pua.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Burudani ya Muziki kutoka kwa Mjomba Bendi katika kunogesha sherehe za kufungwa kwa maadhimisho hayo.
Meneja Habari na Ushauri wa Taasisi ya John Hopkins Centre For Communication Programme Tanzania Fauziyat Abood akitoa ufafanuzi wa Shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo kwa mgeni rasmi alipotembelea katika banda hilo.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara na Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini.

Thursday, September 29, 2011

SPIKA WA BUNGE MAMA ANNA MAKINDA AMTEMBELEA DK MWANDOSYA HOSPITALINI NCHINI INDIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda akimjulia hali Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya alipomtembelea katika hospitali ya Apollo nchini India ambako Profesa Mwandosya amelazwa kwa matibabu. Hali yake inaendelea vyema
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Seif Shariff Hamad akiwa katika mazungumzo na Prof. Mark Mwandosya na Bwana Rodhey Mohan, Meneja Mkuu wa Hospitali ya Apollo alipofika kumjulia hali Prof Mwandosya ambaye amelazwa hapo kwa matibabu baada ya kuhitimisha ziara yake India iliyomchukua katika majimbo ya Andhara Pradesh, Kerala na Karnataka.
 
Kutoka kushoto ni Mhe. Mohamed Aboud (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili, Zanzibar), Mama Lucy Mwandosya, Bw. Radhey Mohan, Meneja Mkuu wa Hospitali ya Apollo, Mhe. SEIF Shariff Hamad na Prof. Mwandosya
hostgator coupon code