Saturday, October 8, 2011

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ahudhuria Mkutano wa Afrika na Asia katika harakati za kumsomesha mwanamke

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akihutubia Mkutano wa Afrika-Asia 2011 leo ambapo amesisitiza elimu yenye maadili ndiyo njia pekee ya kumkomboa mwanamke pamoja na jamii kwa ujumla. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Wanawake cha Sookmyung nchini Korea Kusini ambacho kimetiza miaka mia moja na tano tangu kianzishwe 1906.
Salma Dinya ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ambaye alialikwa kwenye mkutano huo kuiwakilisha Tanzania kama kiongozi kijana. Hapa anatoa mada kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Asia na Afrika kuhusu Tanzania.
Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Korea katika Vyuo Vikuu mbalimbali walifika kumsikiliza spika wao

No comments:

Post a Comment

hostgator coupon code