Thursday, September 29, 2011

AIRTEL TANZANIA NA ENGEN PETROLEUM ZACHANGIA KUFANIKISHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani, Kamishana Mohamed Mpinga wakionesha stika hizo kwa waandishi wa habari
 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaban Kayungilo na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani, Kamishana Mohamed Mpinga wakionesha stika hizo kwa waandishi wa habari
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta ENGEN kwa pamoja wameungana na serikali ya jamuhuri ya Tanzania kwa kupitia baraza la taifa la usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti namba ya ajali za barabarani nchini.
Leo tumekutana hapa kutangaza wiki ya nenda kwa usalama ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Bukoba. ENGEN Tanzania kampuni ya nishati ya magari nchini Tanzania na Airtel kampuni ya mawasiliano zilikubaliana kuungana na serikali kupitia Baraza la Usalama Barabarani na Jeshi la polisi kuhamasisha jamii kahusu usalama barabarani ili kupunguza ajali.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ENGEN Meneja Bidhaa Jacqueline Kisoka Kupitia SLOGAN ya mwaka huu inayosema “ Usalama barabarani unahitaji uwajibikaji wa kila mtu” ENGEN Tanzania inayofuraha kuwa sehemu ya jitihada za kuokoa maisha ya watu katika jamii yetu na imejitoa kuhamasisha jamii nzima kuzingatia usalama barabarani kama mchango wake katika huduma kwa jamii. ENGEN ni sehemu ya watumia barabara na watumia barabara wengi hutumia bidhaa za ENGEN ndio maana ni mategemeo ya ENGEN kuwa watumia barabara wote wawe salama ili iweze kuwahudumia.
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “kwa miaka 3 mfululizo Airtel kwa kushirikiana na Baraza la Usalama Barabaaarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa. Mchango wetu kwa mwaka huu ni kuchapisha stika na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 2,200 zenye ujumbe wa mwaka huu “Usalama Barabarani unahitaji juhudi za kila moja wetu” .
Matokeo ya ajali za barabarani ni moja ya masuala muhimu kiafya kitaifa. Kila mtumia barabara anahusika awe mwendesha gari, pikipiki au mtembea kwa miguu. Kila mwaka maelfu ya wanaume, wanawake na watoto hufariki kutokana na ajali za barabarani hivyo kusababisha upungufu wa nguvu kazi katika shughuli za uzalishaji kiuchumi. Hii ndio sababu Airtel imejiingiza katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha jitihada hizi”.
Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mallya aliongeza
Note:
Umuhimu wa usalama barabarani hauwezwi kupuuzwa, kila siku tunashuhudia ajali nyingi zikisababisha kupoteza maisha, wa Tanzania wengi, uharibifu wa mali nyingi zenye thamani ya mamilioni. Zaidi ya mguso wa kibinadamu utokanao na ajali za barabarani lakini pia maafa na majeraraha yatokanayo na ajali za barabarani zinaleta athari za kijamii na kiuchumi. Kwa mfano takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa watu 2,850 wanapoteza maisha kila mwaka katika ajali za barabarani. Takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kwamba watu 3,582 walipoteza maisha huku majeruhi wakiwa zaidi ya 20,000 wakati watembea kwa miguu na wapanda baiskeli wakiwa hatarini zaidi.
Mwaka 2010 katika jumla ya ajali 22,750 gharama au hasara iliyotokana na ajali za barabarani zinakadiriwa kufika bil 363. Hii ni athari kubwa kiuchumi.

Monday, September 26, 2011

Petroli, dizeli yapanda tena


BAADA ya bei ya petroli kushuka kwa wiki nne mfululizo, leo bei ya bidhaa zinazotokana na nishati hiyo zitapanda na kudumu kwa wiki mbili zijazo.Safari hii petroli katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh 2,102 kwa lita moja ikilinganishwa na Sh 2,031 kwa bei, iliyoishia jana.

Kupanda na kushuka kwa bei ya nishati hiyo ya mafuta kwa lita, ni sehemu ya utekelezaji wa kanuni ya ukokotoaji inayotumiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).

Wiki mbili zilizopita, Ewura ilitoa bei elekezi ambazo petroli ilishuka kwa Sh38.03 sawa na asilimia 1.84, dizeli Sh 45.15 sawa na asilimia 2.26 na mafuta ya taa bei ilishuka kwa Sh46.15 sawa na asilimia 2.33.

Hata hivyo, jana Ewura katika bei hizo mpya inayoanza kutumika leo imetangaza kupanda kwa bei ya rejareja ya petroli kwa Sh 70.12 sawa na asilimia 3.57 wakati dizeli imepanda kwa Sh 44.88 sawa na asilimia 2.38 na mafuta ya taa kwa Sh 33.02 sawa na asilimia 1.77.

Mkurugenzi wa Petroli wa Ewura, Mutaekulwa Mutegeki alitangaza bei hiyo jana, huku ikionyesha kuwa kwa Dar es Salaam petroli itauzwa kwa Sh 2,102, mafuta ya taa Sh1,967 na dizeli Sh1,999 kwa bei ya rejareja.

Bei ya rejareja katika miji mingine mikubwa ni Arusha ambako petrol itauzwa Sh2,186, mafuta ya taa Sh2,051 na dizeli Sh2083.

Mbeya, petroli itauzwa Sh2,209 kwa lita moja, mafuta ya taa Sh2,074 na dizeli Sh2,106, wakati Mwanza petroli itauzwa kwa Sh2,251, mafuta ya taa Sh2,116 na dizeli Sh2,149.

Sababu za kupanda

Ewura walisema sababu za kupanda kwa bei hiyo ya mafuta ni kutokana na kupanda kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia.

Ewura katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, ilifafanua kuwa petroli imepanda kwa asilimia 5.16, dizeli 2.98 na mafuta ya taa kwa asilimia 2.35.

Pia Ewura imetangaza sababu nyingine, ni kuendelea kupomoroka kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani kwa kiwango cha asilimia 0.55.

Mkurugenzi huyo wa Petroli alisema, kuporomoka kwa shilingi dhidi ya dola ambayo ni fedha ya kimataifa ya manunuzi kumefanya manunuzi ya ndani nayo kuongezeka.

Mchakato kuanzia Agosti 2

Mchakato wa marekebisho ya bei za mafuta, ulianza Agosti 2, mwaka huu ambapo Ewura ilitangaza kushusha bei ya mafuta ambayo petroli ilishuka kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ni sawa na asimilia 9.17, dizeli ilishuka kwa Sh173.49 ambayo ni sawa na asilimia 8.32 na mafuta ya taa yalishuka bei kwa Sh181.37, sawa na asilimia 8.70.

Hata hivyo, uamuzi huo uliibua mvutano kati ya wamiliki wa makampuni ya mafuta na serikali huku wamiliki hao wakitunisha msuli na kugoma kuuza nishati hiyo muhimu.

Lakini, Agosti 10 serikali ilitoa saa 24 kwa kampuni hizo za mafuta kutangaza kwanini yasichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka agizo halali la serikali.

Ewura baadaye ilitoa onyo kwa kampuni zilizogoma ikiwemo Engen, Camel Oil, huku ikimfungulia mashitaka mkurugenzi mkuu wa BP kwa kushindwa kutii amri ya kushusha bei.

Lakini, siku 11 baada ya kushusha bei na nchi kutikiswa na mgomo Ewura ilipandisha tena bei kwa kisingizio cha kuporomoka kwa shilingi na kupanda kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia.

Hata hivyo, wiki mbili zilizopita hadi kuishia jana Ewura ilitangaza kushusha bei tena ya mafuta na kutoa ahueni kwa watumiaji nchini.
Source Mwananchi

Saturday, September 24, 2011

WAATHIRIKA WA MABOMU YA GONGO LA MBOTO WAKIWA KWENYE FOLENI TAYARI KWA KUPOKEA MALIPO YA FIDIA YA NYUMBA ZAO


Baadhi ya wakazi wa Kata ya Majohe Gongolamboto wakiwa katika foleni Dar es Salaam jana ya uhakiki ili kupokea malipo ya fidia ya thamani za ndani na matengenezo ya nyumba zilizoathirika na milipuko ya mabomu iliyotokea kwenye Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) mwezi Februari mwaka huu.Picha Na Majira

Thursday, September 22, 2011

Uholanzi yatoa Sh30 bilioni kugharamia elimu nchini


Tanzania itafaidika na msaada wa Euro Milioni 15 ( zaidi ya Sh30 bilioni ) toka Serikali ya Uholanzi kugharimia mradi wa Kujenga Uwezo kwa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, unaojulikana kwa jina la Netherlands Initiative for Capacity Development in Higher Education(Niche).

Hayo yalibainishwa na meneja wa mradi huo, Ute Jansen, alipotembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro, kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao kwa chuo kikuu hicho, mradi huo unatoa ufadhili kwa Shule ya Biashara na kuboresha mafunzo ya utawala wa Serikali za Mitaa.

Jansen, alisema ana matumaini makubwa sana kuwa mradi huu utakapokamilika, utaboresha sana zile sekta zilizoainishwa kwenye mradi huu ambazo ni kujenga uwezo katika kutoa elimu kuhusu afya, sekta binafsi na Serikali za Mitaa.

Kwa upande wake, msimamizi wa mradi huo Tanzania, kupitia Shirika la NUFFIC, Johanna Van Nieuwenhuizen, alisema Uholanzi imeridhishwa na jinsi Tanzania inavyoitumia misaada toka nchini mwake, hivyo kujihakikishia fursa zaidi za kusaidiwa katika miradi mbalimbali.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Mugishi Mgasa, aliyemwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo, aliishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kufadhili mradi huo na kueleza kuwa ufadhili huo una maana kubwa sana kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe, kwa sababu utapanua uwezo wa chuo hicho katika kutoa Mafunzo ya Biashara na Utawala wa Serikali za Mitaa.

Naye Mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Joseph Kimeme, alisema ufadhili huo, utawafanya wanafunzi wanaomaliza Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, sio tu kuhitimu kwa elimu yenye ubora wa hali ya juu, bali pia watajengewa uwezo wa kujiajiri kwenye biashara zao kufuatia mahitaji ya soko.

Rais Jakaya Kikwete Apokea Tuzo Mbili Maalum Kwa Mchango Wake Mkubwa Katika Afya ya Mama Mjamzito na Watoto,Akutana Na Viongozi Mbalimbali

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihudhuria mkutano wa 'Social Good Summit' anapokea tuzo kutoka United Nations Foundartion for his work in Martenal Health and Social Media Commitment kutoka kwa Makamu wa Rais wa Public Policy of United Nations Foundation Mr. Peter Yeo katika sherehe fupi iliyofanyika jijini New York .
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki- Moon kwenye Makao Makuu ya Umoja Mataifa jijini New York nchini Marekani.Kwa Picha

Sakata La Mkuu Wa Wilaya ya Igunga; Wanazuoni Wa Kiislamu Waivaa CHADEMA


Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewekwa kitanzini baada ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania (HAY-AT) kutoa muda wa
siku tatu kwa viongozi wake wa taifa kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitara yake na kumdhalilisha.


Pia umoja huo umeonya kuwa iwapo CHADEMA hawatafanya hivyo wataandaa maandamano nchi nzima kutangaza chama hicho kuwa adui mkubwa wa dini hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bw. Sherally Sherally alisema kitendo kilichofanywa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA ni udhalilishaji kwa mwanamke wa kiislamu hivyo ni lazima viongozi wake wa juu walaani waliohusika na kuomba radhi.

Tayari watu watatu wakiwamo wabunge wawili wamefikishwa mahakamani mkoani Tabora wakituhumiwa kwa kumshambulia Bi. Kimario na kumwibia simu yake yenye thamani ya sh 400,000. Watuhumiwa hao waliachiwa juzi kwa dhamana hadi Agosti 10, mwaka huu.

Bw. Sherally alisema iwapo chama hicho kitapuuza agizo hilo kwa muda waliowapa umoja huo utapita nchi nzima kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo dhidi ya mwanamke.

"Tunalaani na kupinga kwa ukali kabisa kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa ni wafuasi na viongozi wa CHADEMA kumvua hijabu Bi. Kimario na kumuacha bila stara huko Igunga Septemba 15," alisema Bw. Sherally na kuongeza:

"Kitendo hiki kumvua hijabu Bi. Kimario, kumsukasuka na kumtolea maneno yasiyofaa ni kitendo kiovu sana mbele ya Mwenyezi Mungu, Waislam na Watanzania wote wapenda haki na amani na wanaojiheshimu," alisema.
Katika hatua nyingine Bw. Sherally alisema wamesikitishwa na kushitushwa na kukaa kimya kwa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na wanawake kwa kutolaani kitendo hicho cha mwanamke mwenzao kudhalilishwa kijinsia."Kuendelea kukaa kwao kimya kutatulazimisha kuwaona kuwa wanaafiki na ndumilakuwili," alisema.Chanzo Gazeti Majira.

Wednesday, September 21, 2011

Man city yaweka wazi mpango wake wakujenga "Training Academy Complex"

 
Man city imeweka wazi mpango wake wa kujenga uwanja mpya ambao utatumika kama chuo cha michezo kwa vijana hivi karibuni, Man city ilinunuliwa na bilionea wa Abu Dhabi Sheikh Mansour Bin Zayed Al Nahyan August 2008 na toka hapo amekuwa akiwekeza hela nyingi sana katika kuiinua timu hiyo.
Academy hiyo itakayo jengwa karibu na uwanja wao wa Etihad Stadium, itakuwa na viwanja 15 vya mpira na uwanja utaochukua watu 70,000 wakiwa wamekaa, pia complex hiyo itakuwa na vyumba vya kulala kwa timu 40 kwa wakati mmoja. stay tune for more detail

hostgator coupon code